Tuesday, February 23

Siku Nasri alipoachishwa ziwa!

Mdau Nasri Charunga akifaidi nyonyo la mwisho bila kujua. Hii ilikua December mwaka jana, alikua ana mwaka na miezi miwili, ma'mtu Zena Chande alikua anaenda Nairobi kikazi kwa wiki mbili.

...la mwisho mwisho...

Mama alivyorudi naskia mdau alileta fujo kidogo tu airport maana alitaka kulitoa palepale, lakini alivyofika home akawa ashasahau!

Siku hizi mwendo ni maziwa ya chupa tu....

...utam kunoga hadi mguu juuu!

******
Wadau naomba tusaidiane tips za kuachisha watoto kunyonya, sisi wengine tulitumia kusafiri tulivyorudi wakawa wameshasahau, wadau wengine wanauliza je kama husafiri unafanyaje?

11 comments:

Anonymous said...

Mimi nilimuachisha mwanangu kunyonya alipofikisha miaka 2 na kama miezi 3 au 4 hivi.. Mwanangu alikuwa anapenda sana kunyonya wakati anaenda kulala. Yaani nyonyo ndio inambembeleza. Hivyo nilikuwa ninahakikisha kuwa anakuwa ameshiba kabla ya muda wa kwenda kulala na nikabadilisha zoezi, badala ya kunyonyesha ili alale, tulikuwa tunalala wote.. baada ya muda alizoea.

Anonymous said...

Panakazi hapo?
Watoto wengine hawasahau, mamy hongera sana.

disminder

Anonymous said...

Mimi wangu aliacha kunyonya wakati nakwenda safari Mwanza ya kikazi, niliambiwa na ofisi mtoto ameshakuwa lazima uende. Mtoto wangu alikuwa na mwaka mmoja na miezi saba ilikuwa ngumu na mimi mwenyewe niliumia maana maziwa bado yalikuwemo. Mtoto mwenyewe ndio huyo katimiza miaka minne Joshua mbaba mkubwa sasa. Hongera mama Nasri

Mama Kelvin said...

Du pole mtoto Nasri, mimi Kelvin wangu alikuwa anapenda sana kunyonya ilifika hatua hataki tena msosi anataka ziwa tu, ooh hapo ndio nilipompeleka kwa bibi yake akakaa huko week moja nikaenda kumfata ila nilipomchukua akawa hajasahau kunyonya nikawa napaka ziwa lile arozela sijui chungu kama ua hivi. akilamba anaona chungu akakataa kabisa kunyonya nikaona ningegundua mapema asingeenda kwa bibi yake ningepaka hilo tu asingenyonya.

Anonymous said...

habari naitwa mama Joseph kimono. jose ana umri wa mwaka na miezi tisa. Nilimwachisha kunyonya na umri wa mwaka na nusu nilitumia njia ya dawa ya goodmorning nikapakaza kwenye ziwa alafu nikamwita jose aje kunyonye jose akasema mama pilipili tangu siku hiyo jose ajanyonya tena.Kwasababu dawa ya goodmorning ina laza ya kuwasha mdomoni ndomana jose akasema pilipili Kwaiyo nawashauli wa kina mama wenzangu hiyo ni njia mojawapo na ni njia salama kwa mtoto.
ASANTE.

shamim a.k.a Zeze said...

Lol...i dont think kama Iqra wangu ataweza lisahau...natamani nimuchishe ila namuonea huruma sababu najua ndo kitu kikubwa mimi nayeye kinachotuunganisha, ukizingatia anashinda na dada siku zote za week, siku na akiacha nyonyo si ndo atakuwa hanitaki.....WIVU...lol!!

Anonymous said...

Mimi Brian alijiachisha mwenyewe baada ya miezi sita. Baada ya kutoka maternity leave, alianza kusuasua kunyonya. Akaanza kujiachisha taratibu, ilipofika miezi kama mitano, akazira kabisa nyonyo kwa sababu muda mwingi alikuwa akinywa maziwa ya kopo kutokana na mimi kurejea nyumbani late. Baadaye akaacha kabisa. Hadi leo ukimwonyesha nyonyo anaona kituko anaanza kucheka au analifinya. Sasa hivi ana umri wa mwaka mmoja na miezi saba. Chakula anachopendelea ni MAZIWA; Vyakula vingine tunamlazimisha.

Anonymous said...

naitwa hadija
mimi maryam wangu nilimwachisha akiwa na mwaka na miezi minne,nilipata safari ya kikazi kwa wiki 2.lakini baada ya kurudi wala hajasahau anadai nyonyo. ikabidi nimwache kwamama tena kwa wiki 2, hapo alisahau kidogo lakini hadi leo hii ana miaka miwili akiliona tuu analitaka ,huwa halinyonyi ila akiliweka mdomoni tuu huwa anaridhika

Anonymous said...

naitwa hadija
mimi maryam wangu nilimwachisha akiwa na mwaka na miezi minne,nilipata safari ya kikazi kwa wiki 2.lakini baada ya kurudi wala hajasahau anadai nyonyo. ikabidi nimwache kwamama tena kwa wiki 2, hapo alisahau kidogo lakini hadi leo hii ana miaka miwili akiliona tuu analitaka ,huwa halinyonyi ila akiliweka mdomoni tuu huwa anaridhika

clavery said...

Mwanangu ana miezi 11 na ujUzito mwingine tayari je nimwachishe au aendelee kunyonya mpaka mdogo wake azaliwe?

clavery said...

Mwanangu ana miezi 11 na ujUzito mwingine tayari je nimwachishe au aendelee kunyonya mpaka mdogo wake azaliwe?