Friday, April 16

Happy birthday my angel!

 (X masaa machache baada ya kuzaliwa, alikua na nywele, sijui zimepotelea wapi?)

Leo nasherehekea miaka miwili (2) ya kuzaliwa mwanangu mpenzi Xchyler.
Alizaliwa saa nane usiku, hospitali ya Marie Stopes ya Mwenge.
Kwa kweli ameniletea faraja kubwa sana kwenye maisha yangu, hata siwezi kuelezea.

Nawashukuru wooooote wanaonipa ushirikiano katika kumkuza, shukrani za pekee zimwendee mama yangu, Pyele...hakuna ambacho kingewezekana bila wewe mama.
Shukrani kwa mume wangu mpenzi, Sixtus, pamoja na baba yangu Babu A, na mdogo wangu Anko Alipo.
Pia shukrani kwa ma-anti na ma-anko wote, bila kusahau wadau woooote wa Mama na Mwana.

Karibu na birthday ya mwaka mmoja, alihakikisha anatembea kwa kujiachia, na sasa ndani ya wiki hizi mbili za mwisho kabla hajatimiza miaka miwili anaongeza misamihati kwa kasi ya ajabu, neno tunalolipenda zaidi ni 'KAKAKI' analisema taratibu, lakini anamaanisha hataki! Faraja isiyo kifani.
*****
Tam tam iko, kwa hisani ya BABU (thanks Dady), ila bahati mbaya sijaweza kuwaalika wote, kuna wachache ndio watawawakilisha, mtaona picha Jumatatu.


6 comments:

Elyc said...

Happy Birthday X,Mungu akutangulie kwa kila jambo na akukuze kimo na akili.

Majoy said...

Hongera Mama X, Mwenyezi Mungu akukuzie.

Mama DerrickSammir.

Anonymous said...

happy birthday X may God bless you abundantly hongera baba na mama X kwa kumlea kijana mpaka hapo alipofika tunamuombea maisha marefu na baraka tele
Much love
Mama Ethan Jnr

Mama Kelvin said...

Habby birthday X Mungu akutangulie kwa kila jambo na uwe mtoto mtiifu kwa wakubwa na wadogo, cheza na watoto wenzio vizuri wala usiwapige, najua wazazi wako wanafuraha sana siku ya leo maana wanapata picha miaka miwili nyuma siku kama ya leo walikuwa wanakungoja kwa hamu sana mara Mwenyezimungu akakushusha dunia. waaaaoooh happy birthday X.

Anonymous said...

Hallow Baby X now ur a grown up boy, wish u all the best na hongera mama X kwa kukuza. Ongeza spidi ya misamiati baby boy mbali na kakaki!

Mumy Josh

zena chande said...

happy birthday x, kila la kheri katika maisha yako mungu akukuze, hongera mama na baba x, kijana amekua sas kiukweli, hongereni kwa kukuza mungu awajalie afya njema muendelee kumkuza baby wenu. zena chande