Wednesday, April 14

Msaada: Mahitaji ya kwenda nayo hospitali wakati wa kujifungua

Habari dada Jiang na hongera kwa kutuhabarisha mambo mengi kuhusu watoto.
Naomba msaada wako, mimi naitwa Stella nina ujauzito wa miezi nane naomba unisaidie kama ifuatavyo:
Nikifikia wakati wa kujifungua hospitali natakiwa niende na nini na nini?
Na ajili ya mtoto atakayezaliwa;
Ni vitu gani natakiwa kununu kwa ajili ya mtoto?
Nakutakia kazi njem.

*****
Hello Stella, 
Mahitaji kwa ajili ya mtoto bonyeza hapo kulia kwako, chini ya Bongo Blogs palipoandikwa Mahitaji ya Awali, utapata mahitaji yote yanayotakiwa.
Kuhusu vitu unavyotakiwa kwenda navyo hospitali, inategemea na hospitali, as zingine hawaruhusu umvalishe mtoto chochote cha kwako na wala haiitajiki uende na chochote, wakati kwingine, hadi uzi na sindano utatakiwa ubebe, hapa wadau watasaidia experience zao kwenye hospitali mbalimbali.
Nakutakia kila la kheri, Mungu akujaalie ujifungue salama, tumuone mdau mpya!
Asante, Jiang.

4 comments:

Anonymous said...

Dada hongera na maandalizi ya kukaribisha mtoto, tafuta begi kubwa au sanduku dogo uweke nepi 12kanga doti 3,vijishati vya wachanga unisex vyeupe unafunga tu kwa nyumba sijui jina lake, chupi za mpira 2, kofia kwa ajili ya baridi 2, soksi pair 3, mafuta ya nazi, sabuni ya kuoga mtoto isiwe na kemikali, poda,baby showel 2, viblanketi vya mtoto 5, Taulo.

Kwa wewe mwenyewe Pedi,kanga doti3,nguo za kubadili 4 ziwe na vifungo kifuani kwa ajili ya kunyoyesha, kitenge cha kufunga tumbo 2, chupi 6,sabuni, mafuta,shanuo,ndala za kwendea bafuni, taulo 2.

In case of emergency Spirit, uzi,pamba, mkasi

Hakikisha umefua nguo zote mpya kabla hujamvalisha mtoto au wewe mwenyewe,Sijui nimesahau nini tena maana nimezaa siku nyingi

Anonymous said...

Asante ndugu ulietoa maelekezo.
Nimejifunza mengi sana hapa kwani hata mie nipo njiani ila badobado na ndo mara ya kwanza na sina wazazi.

Samahani kwakukusumbua unaweza kunielekeza kidogo tu suala la uzi, hivi ni uzi gani unaotakiwa? Ni ule wa kushonea nguo au?

Na swali jingine mkasi unaohitajika ni wa aina gani ni mkubwa kwama wa kukatia nguo au vile dogo?

Ninategemea kujifungua katika hospitali zetu za selikari sijui utaratibu wowote.

Natanguliza shukrani.

Mama na mwana Idumu.

Anonymous said...

Wadau hongereni kwa kutegemea watoto, uzi unaweza kuwa wa kushonea au ule wa kushonea sweta maana hasa kama ukijifungua mahali kama sio hospitali basi unatumika kwa huduma ya kufunga kitovu cha mtoto, mkasi tafuta mkasi mpya uwe na makali ya kukata kitovu, hizi ni kwa ajili ya emergency ikitokea kama ukijifungua hospitali hutavitumia, hospitali wanavyao.

Hospitali za serikali ukienda clinic watakwambia nini cha ziada kuleta ukiacha vilivyotajwa hapo juu, kwa akiba yako beba gloves zako mpya kama pea 4, syringe za sindano, usione aibu kumuuliza nesi kwa pembeni utahitaji nini cha ziada wengi watakueleza nini cha kuleta,

Natumaini nimejibu maswali yako vizuri, usisite kuuliza kama una maswali mengine. Jee umeshajua dalili za uchungu na mambo mengine utakiwayo kuyafata ukiwa na mimba?? kama chakula na chanjo??

Alice said...

Yah anony wa hapo juu wa kwanza kaeleza kwa kirefu sana na ameelewesha vema kabisa! asante sana kama nataman tena mtoto vile aah aah inshallah mungu akijalia tena!! but kama up[o dar es salaam njoo duka la watoto linaitwa toto junction utapata malekezo na utapata vitu vizuri kwa ajili ya new baby wanaruhusu hata kuwekeza then siku ukijifungua wanakuletea hapo hospitali wenyewe, wale wana list ipo pale nwahudumu wanakusaidia kuchagua na kukuelekeza pia hata mama mwenye duka atakusaidia kama umekwama zaidi lkn utahudumiwa vema, sina kukumbukumbu za kutosha ila wana wesite yao na kama utashindwa njoo nipigie 0733 660669 nikupeleke!! mie nipo jirani!!

nakutakia heri na afya bora!!

nawapenda wadau wote na wazazi wote!! mungu awabariki