Thursday, May 31

Una diaper free time?

Wamama wa siku hizi aka wamama wa dot com tumerahisishiwa sana.
Vitu kibao vya kurahisisha malezi ya wanetu...tutake nini?
Ila mi nasema hakunaga mwokozi kama nepi za kutupa wengine tunaziita diaper, hata ukiziita pampas we twende tu, ili mradi mwenye duka anayekuuzia anakuelewa na dada anayekusaidia kuzitumia mnaelewana!

Ila kuna issue ya diaper rush (hii hata nepi za enzi zetu ilikuwepo) na UTI (sijui ni kweli kwamba siku hizi imezidi)...haya magonjwa ntatafuta daktari asaidie kuyaelezea, ila je unajua njia nyepesi ya kupunguza kama si kuzuia kabisa magonjwa haya?
(bofya kushoto palipoandikwa ZAIDI BOFYA HAPA,  tu-share njia nnayotumia mie)

Mimi napenda kuita diaper free time ambayo kwangu inaweza ikalast hata the whole day (mchana, sithubutu usiku!!!
Yap, ni Xy anazunguka na kuzurula nyumba nzima bila diaper, yaani akitia kaptura nyepesi au kikufuli chepesi, baaaaasi!
Jamani, na joto lote hili la hapa Dar, na siku hizi naona hadi watu wa Arusha wanalalamika joto, unamwacha mtoto na diaper 24/7?
Duh, yaani haya hapungi hewa? hata ungekuwa wewe ungejisikia vizuri kweli? Hapo ukichanganya na mtikisiko wa kiuchumi, diaper moja 12 hours!!! Si anapikika huko ndani, vile tu haongei.
Unaogopa kuchafuliwa?
Mwonee huruma huyo malaika wako na mpe raha..vua diaper tupa huko kwa masaa kadhaa kila siku utahisi raha anayopata muda huo.
Usijali uchafu wa mkojo, wa utafutwa? afu kama nyumba yako ina tiles sasa unaogopa nini?
Kama ni carpet we mtengee kisehemu chake ambacho hakina carpeti acheze hapoooo hadi afurahi. Kwenye makochi ni NO NO, isiwe sababu ya nyumba kunuka mikojo saa zote!
Mwilini, poa tu, kama uko home si utaoga, na nguo itafuliwa (sivai jeans saa hizo, khanga tu!).
Jaribu weekend hii uona anavyoona raha, afu mwambie dada aendelee weekdays... mie imenisaidia sana kwa bint na bin (hivi hili neno halitumiki hivi) wangu.
Wewe make sure umemlia timing iwe baada ya kujisaidia haja kubwa, ili asichafue sana. 

-Wanasema kizuri kula na wenzio, kibaya tupia.... na wewe tiririka hapo kwenye comments, unatumia njia gani, simple, kuavoid hizo diaper rushes na UTI? 
Afu ukishajaribu wikend hii nipe feedbak, ilikua bombaje?
Una topic/maoni/ ushauri/swali nje ya hii unataka ku-shere nasi? tupia hapa mamanamwana@gmail.com

2 comments:

Anonymous said...

kwa uzoefu wangu pampers hazisababishi uti kama utakuwa unamvua mtoto on time na pia tusitumie pampers na wipes mtoto akienda haja tutumie sabuni na maji safi kusafisha na si wipes

Anonymous said...

Ushauri ni mzuri. Lakini hii kwangu naifanikisha nikiwepo nyumbani, lakini wadada ukiwaambia wasitumi 'pampasi' unakuta mtoto anakaa na nguo yenye mikojo au hata haja kubwa bila kubadilishwa muda mrefu; kisa wanaona uvivu wa kufua. Na wanangu wanapenda kunyonya vidole, kwa hiyo wanajigusa na kunyonya vidole jambo ambalo ni hatari zaidi. Kwa hiyo naona bora tu niingie gharama ya kununua PAMPASI