Watoto wengi
wanapenda sana katuni.
Hili liko wazi na wala halipingiki.
Lakini Mzazi
hivi unafahamu kwamba sio kila katuni ni ya
Sio kila katuni
imetengenezwa kwa ajili ya watoto kama wengi
tunavyodhani. Nyingine ni
za watu wazima.
Wazazi tunapaswa tuwe
makini sana katika kuchagua katuni
za kuangalia watoto wetu.
Kuna baadhi ya katuni sio
nzuri kwa watoto kwa sababu zina vurugu,
matusi na uovu ambao
unaweza kuathiri
makuzi ya watoto.
Ni muhimu kabla katuni
haijampitia mtoto mzazi
aipitie ili aone kama
yaliyomo ni mazuri kwa makuzi
ya mtoto wake.
Na kama utaona yanaathiri
ni vyema kuitupilia mbali.
Mfano wa cartoon ambayo sio nzuri kwa watoto wadogo ni Ed Edd n
Eddy.
Hii ni cartoon ambayo
inawazungumzia vijana (watoto)
watatu marafiki ambao siku zote wanajaribu kuwanyang’anya kwa nguvu au kuwarubuni
pesa watoto wenzao ili wazitumie kununulia pipi. Inshort katuni hii
inawafundisha
watoto kuwa wakatili.
Wazazi yatupasa tuwe makini
katika selection ya vitu ambavyo watoto wetu wanapaswa kuangalia. Sio wazazi
wote tunazingatia hili ndo maana utakuta watoto wanaangalia movie kubwa kupita
uwezo wao. Sio kwenye katuni tu tuzingatie pia hata kwenye hizi Bongo Movies
zetu ambazo ni kubwa kupita uwezo wa watoto wetu.
1 comment:
mdau umenena kwa kweli!
Post a Comment