Friday, August 17

Unaweza ukaacha kazi, uwe mama wa nyumbani aka housewife?


Mzazi mmoja kukaa nyumbani kulea watoto kuna influence kubwa kwenye malezi ya watoto. Yes, kwani anagain nini hasa kwa dada, juu ya usumbufu wa kubadilishiwa dada kila mara? Nna uhakika atafurahia na atagaina zaidi kama akishinda na mama yake au baba yake (hii bado sijaona) kuliko dada. 

Wengine hapa ni product ya mama kula nasi sahani moja, ukinyanyua mguu yeye ameweka hapohapo! 
Dunia ya sasa mamaz wanaokaa nyumbani kulea watoto wanapungua sana. Yap, maisha yanaenda kasi, na pia diploma/digrii zetu tulizozisotea tukazichome moto, tulee watoto?
Ila yote ni mamuzi ya mtu. Nawajua watu walioamua kukaa nyumbani tena wameacha kazi nzuri, kuamua kuea watoto!

Ila mara nyingi siku hizi wanaofanya hivyo ni kwa muda tu, watoto wakianza shule nao wanatafuta vitu vya kufanya; aidha kurudi kwenye ob market, au kurudi shule kuongeza ujuzi au kuwa wajasiriamali!
Na akina baba wanaobaki nyumbani mpo? So far bado sijakutana nae hata mmoja…

Athari za kuwa mama wa nyumbani


Tofauti na masuala ya kifedha, kuna athari zitakazojitokeza zinazopaswa kuzingatiwa. Unaweza kujisikia mpweke kukaa nyumbani pamoja na mwanao unapokuwa katika umri mkubwa. Na kujikuta unajitenga na masuala nyeti kwa kuwa hali hiyo inaweza kusababisha kuongeza kitu kinachotwa postpartum depression. Angalia usije ukageuka desperte housewife!

Kujiamini kwako kunaweza kukuletea athari iwapo hutapata ushirikiano kutoka kwa mwenzi wako na familia kwa ujumla, hasa pale unapokua ushazoea kuulamba asubuhi kwenda kazini. Pia sio kawaida kujisikia upweke na kuchanganyikiwa wakati masuala mengi ya kulea watoto na shughuli za nyumbani yanajirudia na kukufanya mchovu.

Unawezaje kuzuia hali athari hizo?

Japo mengi ya matatizo haya yanatokana na kukosekana kwa mawasiliano ya kikubwa, jenga mawasiliano katika ratiba zako za kila siku.  Kwa lugha nyingine, endeleza mawasiliano kama unavyokuwa kazini lakini lenga kuwasiliana na wengine ambao wanakaa nyumbani wakiwemo akina mama na akina baba wanaofanya kazi part time.


Ufanye nini unapofanya uamuzi huu?

Ni muhimu kuelewa baadhi ya masuala muhimu, yakiwemo, hali yako ya kiuchumi, utashi wako, jinsi unavyowajibika, na muhimu zaidi hisia za kila mmoja wenu anayehusika.  Katika baadhi ya familia, mzazi mmoja kulea watoto kuna maana zaidi.  
Kuna mtu anapenda kukaa home kulea watoto, well some of us tunakimbia kazi za nyumbani! Mwingine anapenda mno kazi yake, ataiachaje? Mwingine hapedi kwenda kazini huku abalance na kulea watoto anajione tabu tu!
Sasa jipime mwinyewe, as there is no wrong answer here! It is up to you  na utashi wako.
Juu ya hapo kuna hali ya uchumi…unaruhusu? Yaani familia kutegemea mshahara au hela ya mtu mmoja inaruhusu? Kama hali ya uchumi hairuhusu hata kama unapenda kulea mwenyewe watoto inabidi uwe mpole tu!

Can you afford kuwa mama wa nyumbani?

Kama jibu lako la kwanza ni ndiyo, unaweza kushangaa. Kama mna uwezo kipesa mmoja kati yenu anaweza kuacha kufanya kazi bila kuathiri mapato ya familia yenu na wakati huo huo kuongeza kuwepo kwako katika kuangalia maisha ya mtoto wenu. 
Suala la msingi hapa ni namna gani inakugharimu wewe kufanya kazi? Ni kutokana na fedha unazopata kulingana na muda unaotumia kuzipata pesa hizo? Kufanya kazi kunagharimu pesa, unapaswa kulipia wadada, vituo vya kulelea watoto aka chekechea usafiri wako na wa mtoto, lunch yako na kadhalika. 
Sometimes mkikaa na kupanga bajeti na kufanya mahesabu kuhusu gharama mnaweza gundua kwamba mmoja wenu anaenda mjini kutembea tu, wala hachangii saana kwenye mapato ya familia.
Ndio, kukaa nyumbani hakumalizi gharama zote kunapunguza tu. Bado unahitaji mavazi, chakula ingawa si sana (wamama mnajua, ukikaa mwenyewe nyumbani matumizi ya home yanapungua sana, as wewe unabalance mahesabu kiujanja kuliko dada), and so on.


Una-save vipi iwapo mmoja ataacha kazi?


Kuishi kwa kutegemea mshahara wa mtu mmoja unamaanisha kupunguza matumizi. Panga bajeti ya kila kitu unavyotumia kwa juma halafu angalia njia za kupunguza gharama hizo. Panga na mwenzako jinsi gani mnaweza kupunguza gharama. Baadhi ya mambo ya kupunguza gharama katika familia ni pamoja na:- 
Gharama za simu: kupigapiga simu kusikukuwa na maana mnaamua kuachana nako!
Beer: mambo ya kukaana washkaji kwenye viosk unayapunduza.
Michango ya harusi: si utani hivi vitu ni gharama. Amua kuchangia watu wa karibu sana na wewe, wenine unawatosa tu!
Outings: badala ya auting kila wikend, mnaweza kuamua kuwa kila mwezi. Achana na maisha ya watu, anagalia ya kwako!
Nguo mpya: unahamia kwenye mitumba ya bai za kawaida. Afu mambo ya kutopitwa na fashion unaachana nayo, narudia tena, angalia maisha uliyochagua kuishi, ukifata ya kwenye bongo muvi utaumia!


Siku nyingine ntazungumzia aina zote za malezi ya mtoto, faida na hasara zake...nakusanya data!
1 comment:

Anonymous said...

Jamani me natamani sana niache kazi nilee wanangu ila tatizo linakuja me ndo ninakipato kikubwa sana kuliko mwenzangu yaani yeye hata robo ya mshahara wangu hajafikia ni ile tu me sikupenda ashinde nyumbani sasa me nikiacha kazi si tutashindwa hata kuwalea hao watoto? na yeye sio mvivu ila me sipendi kwakweli eti yeye ndo ache kazi nogopa jamii itakayvo nielewa na kwakuwa ndugu zetu wanajua me ndo ninakipato kikubwa siwatasema nimemfanya houseboy ni hayo tu ila natamani sana kulea wanagu na wala sio mvivu wa kazi za nyumbani