Wednesday, December 26

Azimio la haki za watoto




Kumekuwa na matukio mengi ambayo tumekuwa tukikutana nayo yanayowakabili watoto. Watoto wengine tunakuwa tunawafahamu na wengine hatuwafahamu.
Watoto wamekuwa wakijeruhiwa, wakifanyishwa kazi ngumu katika umri mdogo na pia hata kufanyishwa biashara ya ukahaba.
Pia hata ukifatilia swala la takwimu idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu (watoto wa mtaani) imekuwa ikiongezeka kadri siku zinavyokwenda. Lakini inawezekana wote hatujui sababu ya mambo hayo. Katika kuperuzi peruzi mtandaoni nilikutana na kitu kinachoitwa Azimio la Haki za watoto baada ya kusoma na kumaliza niliamini kuwa endapo maazimio hayo 10 yote yatatekelezwa Ulimwengu utakuwa Better place for Children to live.

BONYEZA KUSHOTO TUYACHEKI MAAZIMIO NA TUYAJADILI



1.       Watoto wote wana haki ya kupata/kupatiwa mahitaji yao bila kujali rangi,   jinsia, lugha, dini, wapi walipozaliwa au ni nani aliyewazaa.  

2.       Wana haki ya kukua na kukuzwa kimwili na kiroho wakiwa katika afya njema, kuwa huru na mwenye utu.

3.       Wana haki ya kupatiwa majina na kuwa mwanachama wa nchi.

4. Wana haki ya kupatiwa malezi maalum na ulinzi, malazi na huduma za afya.

5.       Wana haki ya kupatiwa huduma hata kama ni za mahitaji maalum kama ulemavu.

6.       Watoto wana haki ya kupendwa na kueleweshwa na jamii nzima ikiwepo wazazi na wanafamilia, pia serikali inaweza kuingilia kati pale inapoona hawajapatiwa na wanazistahili. 

7.       Wanahaki ya kwenda shule na kupatiwa elimu, kucheza na kuwa na nafasi sawa ya kujifunza na kujiendeleza. Mzazi una majukumu kuhakikisha mtoto anapata elimu na  mwongozo wa yale anayoyahitaji. 

8.        Wana haki ya kuwa wa kwanza kupatiwa msaada pale tu wanapohitaji.

9.       Wana haki ya kulindwa dhidi ya ukatili na unyonyaji.

10.   Wanapaswa kufundishwa kuhusu amani, maelewano, kuvumiliana na urafiki na watu wote.
Unadhani nini kifanyike ili haya maazimio yaweze kutekelezeka?

No comments: