Monday, January 19

Mdahalo: Watoto Wanapunguza Mapenzi kwa Baba

Xchyler akiwa amejipumzisha zamani zilee, hata sikumbiki alikua na umri gani.
***
Suala hili limekua likisemwa kwa muda mrefu sana, hata kwenye jiko pati kinadada huwa tunaambiwa 'first born wako ndio mume, usimsahau ukizaa mtoto, maana huyo ndio mtu muhimu zaidi kwako'.
Mdahalo wa wiki hii, hivi ni kweli mtoto anapozaliwa anafanya mama apunguze mapenzi na attention kwa baba?

Najua kina mama mna mengi ya kusema, ila kina baba mna mengi zaidi, ukumbi wenu...

2 comments:

Anonymous said...

Ukweli wa mambo, ni faraja mno na burudisho la pekee mungu akikubariki mtoto. Yaani, hasa ukishafika nyumbani baada ya kujishughulisha na ujenzi wa taifa. Ni mengi huyapata kutoka kwa watoto na sijui nieleze ni hali gani unaona once ukiwa karibu na mtoto wako.
Ina tegemeana ni kivipi unasema kuwa kina mama wakipata mtoto, humsahau mume.

Yaani kuwapa priority watoto, lakini kwa upande wangu naona kama hivyo sivyo. Kwani ni muhimu kuwapa pririty watoto kwani hatujui ni nini wanataka. Yaani tunafanya kubuni , aah vipi ana umwa au ananjaa au ... So bila kuchukua tahadhari namna hiyo na kuwa na makini na watoto wetu, ni rahisi mtoto kushambuliwa na chochote kile pasipo jua. Mungu atuepushe na hayo.

Maoni na ushauri mengineyo, naona nitajaribu kuyatafakari na kuyaingiza au kuchangia kwako nitakapo pata muda, kwani kwa sasa nipo kazini. Ni mgeni kwako na natumai ni mengi tutayajua kutokana sisi wazazi kuchangia mada au kutoa elimu ili vijana wetu wakue vyema.

Wako Baba Junior,

Anonymous said...

True mapenzi yanapungua ila wka miezi ya mwanzo kwani kuzaa kunabadilisha hata the way woemn think. Mawazo yako yotee yanawaza baby wangu sijui hiki sijui kile so yap yanapunguaaaaaaa