Wadau mbalimbali wamekua wakinitumia mails kuulizia maswali ya vitu walivyokosa katikati ya wiki kuhusu topic hiyo ya lishe, Mama Iqra (Babu A anakusalimu) ni mmojawao, so nimeamua kupost hii ili kuwaelezea tena kwamba unaweza kuzipata postings ambazo zilikupita, kwa kubonyeza label ya Lishe hapo kulia (sorry, mwanzo niliandika kushoto), ambapo atapata zooote zilizitoka.
Ila wadau lazima niwalaumu kwa kutonitumia picha za watoto wenu wakipata msosi nilizohitaji kuambatanisha na postings hizo.
I hope next topic mtatuma picha nyingi zaidi. anayetaka topic yeyote tuwasiliane ili nipost kwa manufaa ya wadau wooote.
****
NB: Wadau wa mwanzo si mnakumbuka ile poll kuhusu watoto watahiriwe lini?, Basi kaeni mkao wa kula as poll mpya ya kupigia kura inakuja...we uwe unaangalia upande wa kulia tu.
1 comment:
Kwakweli tunashukuru sana blog hii, experience na mafunzo ni mengi tumepata.
Sasa, nilikuwa nakuomba Jiang if possible utupe mafunzo ya maziwa ya ng'ombe kwa watoto wetu hawa, ni katika umri gani mtoto yu tayari kuanza maziwa ya ng'ombe ninavyo fahamu madr wengi wanatukatalia kuwapa, ila si mbaya tukishauriana pia wazazi kwa wazazi tukaelimishana.
Good day!
Mama A.
Post a Comment