Friday, May 22

Ervin Anapenda Tangazo la Duh, eeh bwana wee!

Huyu ni ERVIN CHONYA (9 mnths) ana wapa hi watoto wenzake woooote anawapenda pia.
Mama yake anasema Ervin anapenda sana tangazo la TIGO Duuh eeh bwana wee!! Pia huwa ana smile akimwangalia msoma taarifa ya habari kwenye TV, sasa sijui anahisi anasemeshwa yeye!!!
Na mimi nauliza hivi kuna mtoto hapendi matangazo ya tigo? X alipenda kuanzia lile la wababu wanacheza, naye akawa anacheza nao, hadi hili la Duh, anaimba nao. Wazazi wengi ninaokutana nao wananiambia watoto wao wanapenda matangazo ya tigo, yanafurahisha kwa kweli, hata sisi wakubwa tunayapenda!

4 comments:

Anonymous said...

HE ERVIN!!! MTOTO WA RUTH MAGESSE CHONYA, JAMANI KAKUA KWELI WATOTO HAWAKAWII KUKUA JAMANI JUZI TU. MUNGU AKUKUZIE MWAYEGO!! by mdau CHRAGG!

Eugene Chonya said...

Mimi ni Baba wa Ervin, Yeye anapenda sana kucheza na kufurahi kila wakati. Kuna wakati unatoka kazini umechoka na unachofikiri ni kufika nyumbani na kupumzika. The moment ukifika nyumbani ukakutana na Ervin oooh! atakakufurahia na kukufanya ucheze naye na ukasahau uchomvu wote. Napenda Ervin na muombea kwa mungu awe na mafanikio katika maisha yake ya baadae.

Anonymous said...

Hongera kwa kuwa na mtoto mwenye afya nzuri. Watoto wanapata faraja sana kuwa na wazazi wanao wajali hasa katika suala la kucheza nao.

Wazazi msichoke kuwa nao jirani, na tuachane na fikra potofu eti mtoto acheze na watoto wenzake tu! Si kweli. Baba wa mtoto lazima uwe na muda wa kuwa busy na mwanao.

Big up wazazi wote wanao penda kucheza na watoto. Nimependa sana.

Anonymous said...

wow what a cute baby!! mimi nina mtoto mmoja alishatokea huko nyuma ni Samora Jr. Tena amepishana siku chache tu na Xchyler. Yeye ni 21/April/2009. sasa na Sam Jr na hayo matangazo ya tigo, zain, voda, pepsi na taarifa za habari anapenda mmo. kweli watoto wanapenda sana matangazo nafikiri kwa kuwa ni kitu ambacho wanaona mara kwa mara.