Friday, May 8

Feni na Mtoto

Mtoto akiwa amelazwa sebuleni kwenye hewa ya kutosha

*****

Najua watu wengi wanaona, na mimi nikiwa mmojawapo, kuwa feni inasababisha magonjwa ya vifua kama mafua na kikohozi lakini utafiti unaonyesha kuwa feni inamsaidia mtoto, hasa kwenye vyumba ambapo hamna hewa nyingi.
Utafiti huo uliofanywa Califonia kwa jumla ya familia 497 kiila moja ikiwa na mtoto mchanga uligundua kuwa matumizi ya feni yalipunguza uwezekano wa vifo vya watoto visivyojulikana chanzo chake kwa asilimia 72.
Kati ya familia hizo, 185 zilikua zimeshafiwa na watoto kutokana na ugonjwa huo ambao kitaalam unaitwa SIDS, na wataalam waligundua kuwa watoto hao walikua wanalala kwenye vyumba ambavyo havikua na mzunguko wa hewa wa kutosha. Vifo vya SIDS huwa vinatokea watoto wakiwa wamelala tu, na hadi leo, ingawa research zilianza tangu miaka ya 80, haijulikani sababu ya vifo hivyo.
Moja ya njia ya kuzuia au kupunguza vifo hivyo ni kulaza watoto wachanga kimgongo (chali), badala ya kitumbotumbo (kifudifudi), na kuhakikisha kuwa chumbani anakolala mtoto kuna hewa ya kutosha au kutumia feni, ila usimwelekezee mtoto.

Posted by Picasa

5 comments:

Anonymous said...

mh ndugu zangu mliopo nyumbani muweke sofa zinazoendana na hali ya hewa ya joto

Anonymous said...

hebu tueleza sofa zipi zinaendana na hali ya hewa gani? mana hapo comment yako inakua haijasaidia

Anonymous said...

kwakweli toka nimetoka labour mpaka leo natumia feni chumbani na mwanangu kifua hakimsumbui, saivi ni ana zaidi ya mwaka m1. joto sio zuri, muhimu tu usimwelekezee mtoto ile feni, kama mimi hua naiacha ipepee bila kuzunguka, yani naifix direction moja tu, na nina hakikisha haiko directly towards mtoto

Anonymous said...

usichokielewa ni kipi wakati unaona sofa hiyo ni ya ngozi au leather na inatakiwa sehemu ya baridi

Anonymous said...

jamani watu tusitoke nje ya topic, masofa hayo ya ngozi feki yamejaa kibao bongo, na sijaona mtu aliyekufa kwa kuyakalia!
nakubaliana kabisa na umuhimu wa feni au hewa ya kutosha chumbani kwa mtoto, maana wengine wakisikia feni tu, utasikia inaleta inaleta nimonia, watu wanajifanya health experts wakati hawajui kitu!