Saturday, May 23

Feza Boys' Wametutembelea Leo

Leo ofisini kwetu (kwa wasiojua ni Tanzania Standard Newspapers-TSN- wachapishaji wa Daily News na Habari Leo) tumetembelewa na wanafunzi wa Feza Boys' Secondary School wakiwa wanafanya study tour, nia ikiwa ni kujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji wa magazeti yetu.

Hapa mwandishi veterani, Mama Ichikaeli Maro (huyu ni mama wa watoto watatu) akiongea na Alkarim, Benjamin, Magambo, Lutfi na Ally.

Kuelekeza kwa vitendo, ni Basil Msongo (baba Brian) akiwa na Kone, Adban, Nasekile, Deni na Kheri.

Grahpic desiger Jacquline Sadiq (mama Jayson) akielekeza jinsi ya kusanifu gazeti kwa Khalid, Aminiel na Robert.

Godlove na Hamidu wakiwa wakisikiliza kwa makini Graphic designer mkuu wa Daily News, Elias Maluba (kwa nnavyojua huyu bado sio baba'ke mtu) akiwaelekeza jinsi anavyopamba kurasa za Daily News.

Kevin akiwa bega kwa bega na mama mtarajiwa (si mnaona gauni hilo) Devotha Meela, naye desiger wa Daily News.
*****
Study tour kama hizi ni nzuri sana katika kuwafumbua watoto waone kazi mbalimbali zinavyofanywa na pia wajue kuwa kuna kazi nyingi sana zaidi ya kuwa daktari au mwanasheria, so wanasoma huku wakijua kuwa kuna options nyingi za kazi.

1 comment:

Anonymous said...

hivi mama x, huku TSN si ndo anakafanya nassara peter? au nassara mswala, nilisikia kapata baby, sijamuona long time kweli, namani nipate picha yake, toka enzi zile za shule jamani