Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mtoto Mariam Isihaka(8) aliyelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke baada ya kuathirika kwa mshtuko kutokana na ajali hiyo. Pembeni aliyeketi na Mtoto Miriam ni mama yake Husna Selemani mkazi wa Mtoni Mtongani, jijini Dar es Salaam.( Habari hisani ya Maisha Picha na Freddy Maro)
*****
IDADI ya watu waliopoteza maisha baada ya mabomu kulipuka katika ghala la kuhifadhia silaha la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni utata, ila si chini ya 18.
Magazeti ya leo yametoa idadi tofauti, kuna wanaosema ni 18, wengine wanasema 19, na wengine 20.
Hospitali ya Temeke jana ilithibitisha kupokea maiti 13 waliotokana na milipuko hiyo, miili tisa (9) ni ya watoto iliyookotwa katika mto Kizinga eneo la Mbagala.
Kwa mujibu wa JWTZ askari sita walikufa katika milipuko hiyo ya mabomu iliyounguza ghala la silaha.
Rais Jakaya Kikwete amesema, ghala hilo halikujengwa katika makazi ya watu, kwa kuwa lilijengwa mwaka 1976 nje ya makazi hayo.

Mama na Mwana inatoa pole kwa wote waliathirika na janga hilo.
No comments:
Post a Comment