Monday, May 4

Unajua Jumapili hii ni Mother’s Day?

Mother’s Day ni sikukuungeni kidogo, hata mimi nilikua siifuatilii sana, ni wiki iliyopita ambapo mdau Maulid Ahmed alinishtua kuwa imekaribia.
Kwa wale wenzangu na mimi waliokuwa wanaisikia sikia tu, au ambao hawajawahi kuisikia nikaona inatuhusu haswa wadau wa blog hii, hivyo basi niwahabarishe nanyi muhifahamu.
Mother’s Day, naogopa kuitafsiri nisije nikapoteza maana, ila inamaanisha siku ya mama, sio ya kinamama, ni sikukuu ambayo ilianzishwa na mwanzoni mwa karne iliyopita na mwanamke anayeitwa Anna Jarvis ili kila familia ipate kutoa heshima kwa mama yao, ndio maana haiitwi siku ya kinamama, ila siku ya mama, yani kila mtu anamtukuza mama yake.
Nchi nyingi duniani, kuanzia USA ilikoanzia zinasherehekea sikukuu hii jumapili ya pili ya mwezi May, kwa hiyo mwaka huu ni tarehe 10.
Kama kawaida yetu, na hasa ukizingatia sikukuu hii, nakaribisha kila mdau kutuma salamu za dhati na upendo kwa mama yake.
Karibuni.

No comments: