Tuesday, May 12

X Anatembea...Kama Penguin

Wadau mchekin X anatembea bila kujishikilia, hii aliianza siku mbili baada ya kutimiza mwaka mmoja, 18/4, na tulishachoka kusubiri, maana kutembea kwa kujishikilia alianza zamani sana.

Jinsi anavyotembea ni vituko tu, bado hajamaster, ingawa yeye anajiona amefika maana hadi mbio anatimua. Bibi yake anasema anatembea kama penguin (ndege wa baharini) so siku hizi tunamtania penguin boy, maana ukiangali kuna ukweli ndani yake.

Bado kuongea maneno yanayoeleweka tu, maana hayo yasiyoeleweka kayaanza zamani sana, hadi nyimbo anayaimbia, za bongo fleva... na Keyshia Cole, hiyo ni juu ya single yake aliyoitunga mwenyewe tangu mdogo!

4 comments:

Anonymous said...

Safi sana, napenda steps za mtoto anapoanza kutembea, watu tunatoka mbali. X sio muoga anatembea kwa uhakika sasa hivi ataanza kukimbia.

Anonymous said...

Am soo dissaponted how Wewe Mum like you Mkristo hujui Mdomo Unaumba my love dont call little Boy Penguine Boy akiwa Mkubwa na vitabia tabia vya ajaabu mnasahau mlimwitaga Penguine Boyyy shaurilo bibi habari ndo hiyoooooooooooooo

Anonymous said...

nimecheka sana kuona kuna watu wenye imani zakijinga miaka hii mdomo unaumba, basi watu maarufu na watoto zao muda huu wangekuwa mawe kwasababu wanasemwa kila siku kwenye magazeti na tv,tabia ya mtoto inatokana na malezi kama umemlea mtoto wako vibaya atakuwa anatabia mbaya tu hata ukimuita malaika kila siku ,

Anonymous said...

Mum X uminiangusha iz not Imani I swear amini huo Utandawazi ndo unakudanganya anagalia Mdomo Umkristu wewe?Eti Imani Unatakiwa kumnenea mwanao mema hiz TV zinawadanganya mnasahau mlikotaka ata mtoto ukamlea na maadili kama unamwita Penguin likija kuwa kubwa akili hamnazo litembea kama Bata utasema Imani?Mrudie Mungu wako Mimi nimekusamehe Mara 70 kuna Msemo Usilolijua ni kam aUsiku wa Giza utamleaje mwanao ktk Maadili wazazi wa siku hiz twasaka Pesa hakuna Elimu Bure mama unarudi jion Mtt kalelewa na Housegirl Usijidanganye