Thursday, June 18

Kajishule Kamechanganya

Wadau haya ni matokeo ya haka kajishule huku Berlin, hivi vitu nilikua siwezi kuvifanya sasa naweza...tuna Xchyler mapacha, mpole na mtundu!
Wadau wengi wanauliza haka kajishule ni ka muda gani, ni miezi miwili tu, na hii ni wiki ya pili, so by mwanzo wa August ntakua nimesharudi.
Pia wadau wengine wanataka kujua kama nimeenda na X, hiyo ingekua raha sana, ila X kabaki na bibi na baba, so nammiss kichizi.
Jana niliongea nao wananiambia siku hizi anajua kusema baba na kusema sitaki, akimaanisha hasa kuwa hataki hicho kitu, maana kama ubishi karithi kwa baba na mama.

5 comments:

Anonymous said...

Anonymous said....hongera kwa kazi uifanyayo mungu akupe nguvu na ufanikiwe zaidi.

Anonymous said...

MAMA KAILER HUJANIJIBU, KIATU CHA MWANAO NKIPATE WAPE JAMANI, NAKIZIMIA, YANI MWANGU ANAPEA KUMI14 ILA NKIONA KIZURI TU NATAMANI, INGAWA NAJUA KITAMRUKA KESHO, I THINK AM JUST CRAZY ABOUT BABIES' SHOES

Jiang said...

Samahani mdau, ila hiki kiatu hata sijui kimenunuliwa wapi, maana ni baba yake alimletea alipotoka sauzi, kwa bongo sijui kinpatikana wapi. Mama X.

Anonymous said...

hivyo viatu sina hakika kama unaweza kuvipata bongo, na kama vinapatikana basi ni vile made in china, ambavyo tunajua ubora wake. nakumbuka nilinunua huku ughaibuni kwaajili ya wanangu, yaani kuviona tu walijua tofauti yake na made in china, walipovijaribu basi ikawa ishu kuvivua, waligoma mpaka walipolala ndio tukavivua. watoto wa siku hizi wanavijua vitu vizuri, wazazi tujitahidi ili wafurahie maisha.
baba wa kaka zake Livilindu mdogo!!

Anonymous said...

yaani jiang na sixtus na X

mnalipa kinomaaa,perfect family na Mungu awajaalie zaidi na zaidi kwakweli

nampenda X nataka niwe anty yake