Thursday, September 24

X Mbinga

Hapa ni tulivyofika tu Songea mjini, dogo aliingia bila wasiwasi, si yuko kwao.

Hapa ni Mbinga mjini, kuelekea kijijini, kijiji kinaitwa Litembo.

X alipofika kijijini kwa bibi wala hakushangaa, alijiunga na watoto wa pale katika kufanya fujo za kila aina, na kwenda kila sehemu, yani ungemkuta usingedhani ni mgeni, alikua mwenyeji mara moja!

Dogo alikua mchafu sana, maana alikua anadondoka kwenye vilima vyenye vumbi ya udongo mwekundu.

...na alikua yuko kila eneo la tukio, analohusika na asilohusika, alipoitwa na hata akifukuzwa.
Hapa hakukubali hadi alipoondoka na kiazi kimoja mdomoni, kibichi hivyohivyo.
Kiufupi alienjoy sana, na mimi nashkuru wala hakupooza, wala hakuonyesha uchovu wa safari, kwa hiyo hatukuwa na wasiwasi wa kusema labda anajisikia vibaya au ana tatizo, safari ilikua nzuri sana.

4 comments:

pam said...

du huyu mtoto wako kama amekua ghafla? as kama last time kwenye picha za juzi juzi tu hakuwa hivi...haya sasa mumtafutie mdogo wake jamani atadeka sana haya msalimie baba yake as kumbe ni my mtani bwana

Elyc said...

Jiang mwanao mtundu sana,huyo dada huko nyumbani anakoma maana nahisi wanakimbizana kuanzia chumbani hadi jikoni,vurugu mtindo mmoja! Hongera kwa kukuza

Anonymous said...

safi, jamani ilibidi kumpeleka na Liganga aka Putire, huko ndiko mahoka yaliko. au mnasemaje wenyewe! kule Litembo ni wahamiaji kutokana na kazi, ila Liganga ndio makazi yenyewe!!!

Anonymous said...

huyu X anaonekana mtundu jamani na amekuwa haraka