Monday, March 8

Happy birthday Iqrah

 Beautiful Iqrah....malaika wa ukweli!
Jana ilikua siku ya kuzaliwa ya mdau Iqrah, ambapo alitimiza mwaka mmoja (1) bahati mbaya niliingiza siku yake ya kuzaliwa vibaya, ikawa inaonyesha wiki ijayo, samahani mdau Iqrah, ila halijaharibika neno maana kwenye party blog ya watoto hatukukosa!

 
tam-tam zilikuwa nyingi (kama ne hivi), hii ndiyo iliyokatwa...mi ndio maana naziitaga tam-tam, hii hata kwa macho tu inaonekana tam!
...kama kawa X haishi vituko, akataka kunyofoa kimkono cha keki nyingine ya mdoli, kabla hata keki hazijaanza kukatwa, ila nilimuwahi!


kisu mkononi...kata keki tuleeeeeeeeee....kidogo ilingane nae urefu!

ma'mtu Shamim aka Zeze akisaidia zoezi la kukata tam-tam...


...uma unachelewesha mambo, birthday girl anaiwahi kwa mkono!

 
beautiful...mi nilishasema siku aliyozaliwa kuwa Zeze katuletea fashonista, ona sasa hapa ni mwaka mmoja tu tayari ana swaga za kijanja!


X akilishwa keki! kwa tam-tam tena, hakosi!
Hiyo inayoonekana hapo kulia, iliyoandikwa 'Happy Birthday Iqra' ndiyo ilitaka kunyofolewa kimkono na X!

huyu anayelishwa hapa ni fashonista mwingine, na ma'mtu aliyembeba hapo, ukiwaona wanatembea wote utajua tu, she got it from her mama!

 

 

 
 mafashonista walikua kibao....beautiful little angels...

na wakaka pia walikuwepo wengi tu.

 
pozi za mama ehe...
birthday ilikua booooomba, wadau walienjoy sana, walicheza mno, maana Merry Brown si mchezo, pale ndio penyewe kwa wadau, na wazazi pia tulifurahi, maana na sie tulipata nafasi ya kukutana. Thanks Zeze kwa kutualika.
Picha zaidi mcheck ma'mtu, Zeze HAPA

*****
Mama na Mwana pamoja na wadau wooote tukutakia Iqrah maisha mema, marefu yenye kheri na fanaka tele, Mungu akujaalie sana. 




10 comments:

Anonymous said...

Happy b'day baby Iqra. Like mother like daughter, kamependeza, watoto wamependeza na mama uko juu! mama Rispa

Anonymous said...

Happy Birthday Iqra.
Hongera Zeze umekuza.


hayo maugonjwa kuna usalama wa meno hapo?


disminder

Mama Kelvin said...

Hongera zeze umekuza yaani katoto naona kama amezaliwa juzi juzi tu.

Mama Kelvin said...

Jamani wadau naomba mniambie hiyo ni sehemu gani nimeipenda ilivyopatengeneza vifaa vya watoto kucheza.

Anonymous said...

ingawa sikuwepo but i miss it!! thanks wadau kwa kutuwakilisha jamani ! yaani merry brown is everything for any child, yaani ni mwisho wa yote!

asante kwa picha nzuri!!

love you all
alice
mom of jj

Anonymous said...

hongereni,

TUNAOMBA MJIBU SWALI BASI MERRY BROWN IKO WAPI?

Anonymous said...

kwa wale wanao uliza ilipo merry brown .iko masaki wapenzi ingawa sijui kuelekeza ila naimani mtanielewa ukifika pale kwenye kilima ukisha kishusha kile kilima endelea kunyosha mpaka unakutana na merry brown mkono wakulia ,

Mama Kelvin said...

Asante mdau uliyetupa maelekezo ilipo Merry Brown

shamim a.k.a Zeze said...

NASHUKURU SAANA WADAU JAMANI, NASHUKURU KWA DUA ZZENU.....PARTY ILIFANYIKA MARRY BROWN YA MASAKI AS ZIPO MBILI YA MLIMANI CITY NA MASAKI ILA HAPO NI MASAKI, NJIA NAONA MDAU HAPO JUU KASHAELEKEZA NI PAZURI, WATOTO WANACHEZESHWA, WANAPEWA ZAWADI NA UNACHOTAKIWA KULETA NI CAKE NA MSHUMAA, MIE NILISAHAU MSHUMAA LOL NA BEI ITS AFFORDABLE .

Anonymous said...

shamim you did a great thing kuleta watoto with same age kwenye pati ya mtoto wako.sio unaalika watu wakubwaaaa.happy bday baby cake