Siku yetu leo jamani, kama wanawake tuna majukumu mengi sana kwenye jamii na maisha yetu kwa ujumla.
Tunaweza kufanya na kuwa vitu vingi sana, na vingi vyake hata wanaume wanaweza kuvifanya, ila kasoro kimoja kikubwa ambacho kinatufanya tuwe JUU kuliko wao, sisi ndio akina mama.
Iingawa tunashiriki wote wanawake na wanaume katika kutengeneza mtoto, ila ile kazi ya kukibeba kiumbe hicho hadi kiwe tayari kuja duniani, kazi ya kutunza mtoto tumboni miezi tisa ni kazi ambayo ni sisi tu tunaoweza kuifanya, ndio maana nasema tupo JUU! maana si kazi ndogo.
Mimi kama mwanamke na kama mama kazi hiyo nzito wala siichukii, ningempa hifadhi mwanangu tumboni kwangu, hata kama ingekua miaka tisa, maana ni kitu kizuri sana.
Najivunia kuwa mama na siku hii ya leo nawapongeza wanawake wooooote, wenye watoto na wasio na watoto, kwa kuwa wanawake.
Nina role models wengi sana, kila mmoja kufuatana na ninachoona kinanifaa kwangu ila mwanamke nnayemuangalia na nnayetamani niwe kama yeye katika jukumu langu la kuwa mama ni mama yangu mzazi, Mrs Pyele Alipo, nashukuru sana kwa kuwa na mwanamke kama yeye kama mama yangu na najiona na bahati kwa kuwa mwanae. Asante mama.
Siku njema ya Wanawake kwa wadau woooote, wimbo nnaoufeel leo ni Strength of a Woman wa Shaggy hasa kwa maneno haya:
'So amazing how this world was made
I wonder if God is a woman'
I wonder if God is a woman'
No comments:
Post a Comment