Monday, April 11

Ushauri - Nimeconceive, mtoto mkubwa ana hasira, nifanyeje?

Hello Mama wa Mama na Mwana,

Hongera kwa kazi nzuri na majukumu kama mama
Mimi ni mama wa mtoto mmoja mwenye miaka 2 kasoro mwezi. nina tatizo ambalo nahitaji wamama wazoefu wanisaidie.

ni la kisaikolojia zaidi, nimekuja kugundua kuwa nimeconceive kwa miezi miwili sasa, mimi ni mama ambaye nina majukumu sana na nipo busy, huwa sina muda sana na mtoto wangu kama wamama wengine, sasa nina kama mwezi namuona mwanangu anakuwa na kama katabia kahasira sana hasa akiniona, tena niligundua hivyo kabla sijajua kama nimeconceive.

sasa tatizo nilonalo ni ile hali kwamba mwanangu atakuwa hajapata mapenzi na mimi halafu tayari i am expecting another one, so kwa mmama ambaye aliwahi kufikwa na tatizo kama hilo au anajua hayo mambo msaada please wa namna ya kushusha hiyo presha, najisikia vibaya sana i dont have time with my baby and i am expecting.

na nimhudumieje ili asidhoofu, ameacha kunyonya tayari.

asanteni sana.
Mama G...
*******
Jamani wenye experience kama hizo, msaada wa haraka unahitajika.

1 comment:

Anonymous said...

Mama G,Pole na hongera kwa kuconcieve!Mie ni mama wa watoto 2 wakubwa tu, Napenda kukushauri hivi,kwanza jitahidi sana jamani kuwa karibu na mwanao umenishtua unavyosema huna time na mwanao coz upo busy sana Aisee ni mbaya sana inaweza kukucost sana!Wamama karibu wote we're very very busy but tunajitahidi sana kuwa busy pia na watoto angalau masaa kadhaa ujue nini kinachoendelea hata tabia mpya mtoto alioianza au ana kipi kipya! Yaan nakusihi sana kuwa karibu nae sana toka nae mpeleke kwenye michezo ya watoto n.k tena kipindi hichi muonyeshe upendo wa hali ya juu atabadilika na hasira zitamwisha. Isikute hizo hasira zimetokana na kukuona wala humjali au upo busy sana yeye na dada tu imem-bore! Ma'G watoto wana akili kuliko unavyojua, anajua huyu ananijali au kunipenda na huyu hanipendi wala hanijali yote wanajua so BE CAREFULL coz mtoto akikuchukia anakuchukia kweli na wewe ni mama utajisikiaje?
Mama E.