Hello Jiang,
kwanza nakupa hongera kwa kazi unayofanya nafikiri kuwa na kazi ya ofisi,mama wa mtoto na kublog si mchezo,endeleza kasi nzuri.
mimi ni mdada wa miaka 27,pia samahani kama nitakuwa nimekusumbua lakini katika kuangalia nimeona wewe uko very positive na maisha hasa kuhusu watoto,nimejifunza kutotafuta ushauri kwa mtu ambaye ni negative mara nyingi,
sasa tatizo langu ni hili imetokea katika maisha yangu ya mahusiano nimekuatana na mtu tukapendana kwa muda ambao nakiri sio mrefu wa kutosha tukafanya zile habari za wapendanao lakini ile siku tu kumbe haikuwa salama kwangu nikapata ujauzito,kweli nilikosea kukubali kufanya mambo ayo in the first place mbaya
zaidi sikutumia kinga kweli hapo najua nimekosea hasa usinishutumu nimeshakiri
Shida inakuja baada ya kumuambia huyo boyfriend akasema hana muda wa kulea mtoto sasa hivi kwanza anataka kwenda nje ya nchi mwezi wa tano(mambo yakienda sawa wangu atazaliwa mwezi wa sita) kwa sababu hiyo niitoe hiyo mimba, nijibu tu kwamba lakini mbona watu wanalea watoto zao wakiwa mbali akageuka ooh umenitegeshea kulala na wewe siku moja tu umeingia mimba kwani hukujua kama ni siku ya hatari? nikamjibu tu unakumbuka nilivyokulazimisha tutumie kinga ukakataa? hakukubali ukweli, basi uhusiano ukaanza kuyumbia pale siku moja akawa nje ya dar nikaamua tu kutoka moyoni nikijua atakuwa na msimamo tofauti,najuta hata kwanini niliwasiliana naye siku hiyo,akaniuliza enhee vipi hiyo mimba umeishaitoa mimi nikamuambia bado, akauliza kwani ina muda gani nikamuambia ndio inamaliza mwezi inaelekea mwezi wa pili,akaniambia sasa kinashindikana nini si tutoe tu bado ndogo hiyo,nikamwambia siko tayari mi naona kwa sasa sina kipingamizi nitamlea tu huyu mtoto,(nilishawahi kutoa mimba kabla,mungu anisamehe nikaapa sitarudia tena maishani mwangu)
Basi ndio akaniambia unajua sio vizuri kuzaa watoto wawili wakati hujaoa na nilishakuambia mi nina mtoto wa miaka miwili sasa itakuwaje mi nikamuambia sio shida nitaficha tu kwa watu kwamba sitataja jina la baba kama swala ni aibu,akasema hivi kwa nini umengangania nikamwambia mi naona kwa umri na kazi na upendo nilionao kwa watoto sina sababu ya kutoa mimba kwa sasa,akaniambia sasa sikia nikuambie nina mke ana mtoto mmoja na nategemea mwingine mwezi wa pili (huu tuliopo) na kama naendelea na msimamo wangu fine lakini hataweza kumtunza mwanangu na wala nisimtafute tena anafurahi tumejuana hawezi kuvunja ndoa yake kwahiyo ananitakia maisha mema, siku ile nilikuwa kwa rafiki yangu vinginevyo hata ningeweza kuanguaka na kuzimia kabisaa uchungu wake siwezi kuelezea kiufasaha,rafiki yangu akaniambia usitoe kaza roho mtoto utamlea tu yeye(rafiki ameolewa)
basi ukichanganya na maamuzi binafsi niliyochukua nikaamua kulea tu huu ujauzito peke yangu nimeendelea nao weee lakini huko kazini hali mbaya siitwi tena kwenye projects kama zamani yani nimechacha mpaka sasa nimetafuta kazi wee mpaka nimeishia kukubali kazi za kawaida sana hivi ninavyoongea mimba inaelekea kutimiza miezi mitano lakini honestly siko stable kifedha na baba mtoto hanibip wala kunisms.
kinachonipa hofu kuna siku nikiamka asubuhi moyo unaona nimeelemewa nakata tamaa ya kila kitu naona sitaweza naishia kulia tu lakini baadae najipa moyo ila naona kama inazidi sasa yani sina uhakika na maisha tena yani sijui hata nisemeje
ndio maana nakuomba tu ushauri maana mtoto namtaka ila haya mzingira niliyopo naona kama nitapata shida sana kuna wakati najuta sana
hebu nishauri ndugu sijui hata nifanyeje tena
natanguliza shukrani
narudia tena samahani kwa usumbufu