Sijaolewa ila nilikuwa na mtu ambaye amenipa mimba sasa ina miezi miwili, mwanzoni alikubali vizuri kuwa tutailea,ila akachenji ghafla na kunilazimisha nitoe wakati mi siko tayari kufanya hivyo basi ameamua kuniacha niko so diplaced jamani nifanyeje?
Halafu natapika sana naishiwa nguu inanitishia amani hata ya kwenda ofisini ingawa najikokota hivyo hivyo nifanyeje halii hii ipungue nimesha tumia dawa za kuzui kutapika lakini wapi.
Mdau.
6 comments:
Kwanza rekebisha kauli, huo uliyekuwa naye siyo amekupa mimba ila mimba imetokana na uhusiano mliokuwa nao, tena inaonyesha ni wa muda mrefu kwa nini ulikuwa hutumii kinga kama hukuwa tayari kuwa mama?.
Lakini jambo la pili linalotoa wasiwasi ni kwamba huenda hukumshirikisha huyo jamaa yako kama unampango wa kuzaa nae ndio maana ana mawenge, kwanza alikubali lakini kageuka na kukataa hiyo.
Sijajua umri wako ila nina wasiwasi kuwa huenda ukawa ni mmoja kati ya Mabinti wanaoamini kuwa ukipata mimba ndio njia ya kumkamata mwanaume akuoe sio ooo sio wanaume wa sasa.
Ushauri. Mtafute huyo mwenzi wako, mkae chini mzungumze umweleze taratibu na kwa kituo athari unazoweza kuzipata kwa kutoa mimba, pia mwambie ulimuamini atakuwa ni wako milele ndio maana mlikuwa huru kufanya ngono bila kinga.
Lakini usisahau kumpa nafasi ya yeye kujieleza kwanini anadhani utoe mimba, anampango gani na wewe.
ILA USITOE MIMBA KWA SABABU
1. NI ZAMBI
2.UNAWEZA KUPOTEZA MAISHA.
3.UKAHARIBU MFUKO WA UZAZI NA USIZAE TENA MAISHA MWAKO
Maisha bila mwanaume yanawezekana na hata kulea vizuri kuanzia hiyo mimba mpaka mtoto utaweza ikiwa utaamini unaweza.PLAY UR PART IT CAN BE DONE.
Jiang usipotoa hii comment tutagombana ohoo
Pole sana dia!Mimi nakumbuka nilikuwa
natapika sana nilijikaza na sikutumia dawa yoyote!Nakushauri usitumie midawa!hii hali itaisha baada ya 1st trimister!Mimba ndo zilivyo kwa wengine mimi nilikuwa natamani kulia kila ukila unatapika!pia kula sana chakula unachokitamani!
Pole sana mpenzi kwa hayo yaliokupata. Mimi pia nilishakua kwenye situation kama yako......kwa bahati mbaya sikujua nilichokua nafanya, out of anger and frustrations basi nikatoa hiyo mimba and believe me when I say its the worst decision I have made in my entire life, it has been hell for me. There has never been a day go by without me thinking of my baby..... Believe me when I say DONT DO IT!! its not worth anything in your life, the guilt and the pain you go through after that is ubearable.I cry a lot when I think of my baby. She would have been 19 weeks right now. I am always asking God to forgive me.I know I was wrong doing what I did. If I could turn back the hands of time I would never had that abortion.
Keep the baby sweetheart. God gave you that child because he knows you can take care of it, he will see you through this, all shall be well, just trust in GOD. I dont want you to regret and go through what I am going through right now, all I do is WISH but its too late for that now. Dont litsen to what this man is saying to you. Concetrate on your life and the beutiful baby you are carrying.....Be blessed my sister!!
asanteni wapenzi kwa msaada wenu wa mawazo atleast najiskia vizuri na sitomtoa mtoto wangu asante pia jiang kwa kupost tatizo langu thank u guy god bless u.
mdau
nakushauri usitoe hiyo mimba, kwanza wewe unakazi, zaa mtoto wako, kuhusu kutapika hiyo ndio hali ya mimba ila tu jitahidi kula ukipendacho
Pole dia hio ni hali ya maisha watu wengi huwa wanakuwa selfish na wanajifikiria wenyewe usijali huko kutapika saa nyingine ni ule msukosuko wa ile miezi minne ya kwanza baadae huwa inaisha na saa nyingine huletwa na mawazo na kuwa unsettled kama uko kwenye kile kipindi cha mwanzo cha miezi minne ya awali unaweza kujaribu kuchemsha maji ya tangawizi ukanywa ile asubuhi kabla hujala breakfast maji hayo yawe kidogo kama vijiko vikubwa vinne na tangawizi iwe fresh hiyo inaweza kukusaidia kupata mimba sio kosa la jinai kama huyo baba mtoto mtarajiwa alikataa basi usijali tunza mwanao na jitahidi usiwaze wala usiwe unsettled maana hali hiyo itamuathiri mtoto ambaye hajazaliwa mimi tulikuwa na mfarakano na baba watoto wangu baada ya kupata mimba kwa kile alichodai hakuwa tayari kupata mtoto nilishikilia msimamo wangu na kumwambia siko tayari kwa lingine lolote na hata asipotoa hata shilingi mtoto atakuwa kumbuka hapo nilikuwa mwanafunzi tena nje ya nchi baada ya kuona nimeshikilia msimamo wangu ilibidi akubali hali halisi ninaiona furaha ya kuwa na msimamo nimejifungua salama mtoto mzuri wa kiume ambae kwa sasa ana miezi kadhaa siachi kuwaza kama ningefanya abortion ingekuwaje mambo yamebadilika baba haambiwi kitu kwa mwanae anampenda kuliko lakini haya yote yanakuja baada ya kuwa na msimamo wanaume wengine huwa wanafanya hivyo wakijaribu kutaka kujua msimamo wako na hilo ndilo kosa kubwa tunalofanya kina dada kukimbilia kwenye abortion baada ya kuona mambo yamekuwa mabaya Mtunze mwanao na utaiona furaha yake baadae nani alisema mzazi mmoja hawezi kutunza mtoto natamani niongee na wewe uso kwa uso nikushauri zaidi ila kama utaweza wasiliana nami kwa hii email address ruthdavid3@hotmail.com
Post a Comment