Saturday, December 27

Triplets for X Mas

Bi Mariam Rajabu Mkazi wa Mwanayamala A Dar es Salaam, amejaaliwa zawadi tatu krismas hii. Mariam amejifungua mapacha wa tatu katika Hospitali ya Mwananyamala na yupo katika mtihani mzito wa juu ya kuwalea watoto hao watatu ambao mmoja kati yao ni wa kike.Kwa mujibu wa Mariam anasema aliyempa ujaziuzito huo alimkana tangu mwanzo na hamjali kwa lolote na Familia anayoishi nayo pia ni maskini. Na tangu amelazwa hapo hakuna yeyote aliyefika kumjulia hali na anategemea msaada mkubwa wa wauguzi. Anaomba yeyote aliye na msaada wa hali na mali chakula au mavazi asisite mkusaidia ili kumpunguzia ugumu wa kulea viumbe hivyo visivyo na hatia vilivyozaliwa katika kumbukumbu ya kuzaliwa Kristo Yesu au Nabii Isa.
Yeyote mwenye msaada awasiliane na Mroki Mroki wa http://www.mrokim.blogspot.com

3 comments:

Anonymous said...

i agree your idea ! very nice blog

Anonymous said...

Coming to your BLOG, I feel a good start!

Anonymous said...

It seems my language skills need to be strengthened, because I totally can not read your information, but I think this is a good BLOG