Showing posts with label Birth. Show all posts
Showing posts with label Birth. Show all posts

Tuesday, August 13

Karibu Suzan



Mdau mpya ameingia mjini,anaitwa Suzan hapa akiwa na siku nne duniani.nampenda sana baby suzan namtakia maisha marefu.
Mama Suzan.

***
Mama na Mwana inakukaribisha duniani na kwenye playground yetu hii hapa Suzan.

Thursday, October 4

Hongera Siyabonga, karibu Gershon




Mdau Siyabonga Beatrice ambaye amepata mdogo wake Gershon Silver siku ya birthday yake,
Kifupi wamezaliwa tarehe moja na mwezi mmoja(29/06) kasoro miaka..

Mama na Mwana inawapa hongera nyote, Mungu awakuze.

Friday, June 1

New Boy in Town

Amezaliwa mwisho wa mwezi 31.05.2012.

This Sister wa Agakhan Hospital so lovely. Nimempenda sana.

Bibi anamshangilia mjukuu.

Aunt mwenyewe (Mama Cleo) pamoja na baba mtoto.

Tunakifurahia Kidume chetu.

Aunt Irene mwenyewe.


Hope madada watamfurahia sana maana walimngoja kwa hamu mno.

Monday, May 28

Coooongratsss- It is a girl!


Jamani, I cant believe it...huyu ma'mtu, Naomi Lugoe, nilikua naye hapa ofisini muda si mrefu akanipa hi,  tena ya kuchungulia mlangoni...mara naambiwa keshatuletea mrembo...


Congrats sana kwa mama kwa kutuletea binti. Mungu awabariki nyote!

Thursday, March 8

Mdau mpya - Emmanuel




Emmanuel: Kwa wakristo maana yake ni Mungu pamoja nasi.
Alizaliwa Dec 4, 2011.

 Emmanuel ( he is very handsome) na ma'mtu wakipozi. Pole kwa ma'mtu alijifungua kwa C-section.


Like mother like son.

 Waki show love na Cleopatra.( Dada na kaka).

  Mama ya Cleopatra na mama ya Emmanuel ni mtu na mdogoye.

 Mama ya Emmanuel akiwa kwenye safari ya mwisho ya kumngoja mgeni.


 Cleopatra nae hakuwa nyuma kumngoja mdogo wake kwa hamu kubwa sana.

Kila la heri mama Emma katika makuzi ya mtoto.

Wednesday, February 29

X ingizo jipya!

New family member anaitwa Xyleen Lerato Mapunda...hii ni few minutes after birth!
During my time out nimeleta kitu kipya! Huyu ni mdogo wake Xchyler, anaitwa Xyleen (tamka Shyleen) kifupi ni Xy (Shy). So unaweza kuniita 'Mama X squared'.

Kaka mtu, aka Biggie aka X anampendaaaaaa balaaa...! I know for sure anampenda kuliko mtu yeyote!


X alikuwepo tangu mwanzo, alikua anamsubiri kwa hamu huyo mtoto...


Safari yake ilianzia wakati uleeeee nikiwa SA, so ndio maana tukampa jina la kati  la Lerato lenye sili ya ki-Tswana lenye maana ya pendo.
...Pozi la tumbo....



Bize hadi siku ya mwisho...
 Hii ilikua kama siku tatu before kumpokea mgeni huyo...nilienda kazini hadi Ijumaa, Jumamosi mchana nikaenda hospitali, nikajifungua usiku wa kuamkia Jumatatu.





Binti shashiriki matukio mengi ya kifamilia, ikiwamo hii graduu ya dady...
 Kuna walionitumia msg kuuliza kama huyo hapo ni X, yes, ni yeye akiwa na memba mpya wa familia, wakimpa tafu dady kwenye mahafali. (Huyo ni classmate wa dady, Hoyce Temu).




anapenda sana kucheka.

Leo anatimiza miezi sita ya kuzaliwa, so alizaliwa August 29, 2011. Ana kajino kamoja, hiyo picha ya kajino bado sijaipata, maana ni la chini, so kulipata kwenye pozi si kazi ndogo! Katika miezi sita hii kuna mengi ya kusema juu yake, ila mtamjua tu taratibuuu...


...na hapa kwenye bembea yake humtoi!

Of all the things anapenda kula, anything, ila haswa nyonyo!!!
hapa na dady home...

Nashkuru Mungu nimepata shost wa ukweliiii...swali ni nimejizaa au sijajizaa???

Mdau na wewe una update? Iwe la mdau huyo huyo wa zamani tunayemjua au una ingizo jipya we tuma kwenye mamanamwana@gmail.com, maana nimewamisi wadau wangu balaaa!

Tuesday, November 9

Karibu Jonelle

 
 
Mama na Mwana pamoja na wadau wooote  inamkaribisha mdau mpya, Janelle James kwenya playground yetu. Mdau amezaliwa Jumatano iliyopita, Novemba 3. Huyu ni mdogo wake mdau wa siku nyingi sana Jayson James...
 
 Ma'mtu nilikua naye sambamba kwenye ingizo la kwanza -- X na Jayson wamepishana mwezi-- tulikua tunashindana matumbo ofisini...ila hapa nishaachwaaa...

Pongezi kwa ma'mtu Jacqueline Sadik na ba'mtu James kwa ingizo jipya...nyumba ya Js (Jacq, James, Jayson & Janelle).
 
 Hapa mdau yuko na Regina Kumba aka mama Harrieth, ambaye ndio amepiga picha hizi...asante.

Thursday, May 20

Karibu Jenipher

Mama na Mwana kwa niaba ya wadau wooote tunafuraha ya kumkaribisha mdau mpya aliyezaliwa tarehe 5, May mwaka huu, pale hospitali ya Bugando, Mwanza.

Wazazi wake wana .furaha kubwa kwa ingizo hili jipya la furaha kwenye maisha yao. Mdau amepewa jina la Jenipher. Picha hizo juu mbili ni muda mchache, kama dakika tano tu, baada ya kuzaliwa.

Mdau pia ana kaka anayeitwa John, kwa hiyo mama yao, Emmy siku hizi unaweza kumwita Mama J's. Naona baada ya kuulizia watoto no 2, napewa majibu ya vitendo, si maneno, kumbe wadau walikua njiani.
Hapa ni siku ya pili baada ya kuzaliwa...beautiful...Mungu amjaalie mdau na mama mtu afya njema na maisha yenye kheri na baraka tele.

Tuesday, May 18

Karibu Baraka

 Jana tu nimeulizia baby no 2, nimepata jibu toka kwa Edda Mmasi, anasema yeye tayari keshatuletea mdau wa pili.
Malaika huyu mpya, anaitwa Baraka, amezaliwa Ijumaa ya tarehe 30 April.

Cuuuuuuuuuuuuuuuuuute!
Alizaliwa kwa operation, maana alikua 4kg, Mungu amejalia, mdau na mama, Edda Mmasi wanaendelea vizuri. Kaka yake mkubwa anaitwa Prince, ni mdau wa siku nyingi sana hapa kwenye playground yetu.

Hapa kaka mkubwa akinywa soda kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka miwili, ilikua February 2.

tam tam ya pool table...

Party ilikua home, then akaenda kujivinjari South beach, kama anavyoonekana hapo chini...

Miwani imemtoa bomba!
*****
Mama na Mwana pamoja na wadau woooote tunampongeza mamie Edda kwa kuleta mdau mpya wa kucheza naye hapa kwenye playground yetu, pia tunamuombea mdau mpya Baraka, Mungu amjaalie afya njema na maisha merefu yenye kheri na baraka tele amzidi hata wa jina wake Baraka Obama.

Thursday, April 22

Karibu Bella

Pongezi za pokee ziwafikie rafiki zangu, Dr Moses Ringo, aka Dr Mo na Dr Georgina Balyorugulu kwa kujaaliwa kupata mtoto wao wa kwanza, aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo, saa 8.25, hispitali ya Muhimbili.
Mdau huyo mpya anaitwa Bella tutaona picha zake soon!
Dr Mo ana aka mpya, Baba Bella! anavyojidai, utamtaka!
Mama na Mwana pamoja na wadau woooote inamuombea mdau mpya Mungu amjaalie afya njema na maisha merefu yenye kheri na baraka tele.

Thursday, April 8

Congrats: Brianna apata baby sister

Mdau Brianna (pichani) amepata baby sister asubuhi ya Jumapili ya Pasaka, yaani tarehe 4.
Mama na Mwana inatoa pongezi kwa ma'mtu Brenda na ba'mtu Ben kwa ingizo hilo jipya.
Mungu amjalie mtoto mpya maisha mema yenye afya tele.

Jina bado linatafutwa, for the time being ni 'toto', naamini linatafutwa jina linaloanzia na B, maana hao nyumba nzima ni Bs.

Monday, February 15

Karibu Elizabeth Valentine

*Valentine baby*
Anaitwa Elizabeth Valentine (mi ntamwita Liz V), amezaliwa jana alasiri, hospitali ya Agha Khan. Hii picha ni ya leo asubuhi, keshachangamka!

Mama na Mwana inawapongeza Jacqueline na Aaron Suluba kwa ingizo jipya. Huyu ni baby No Two, ana kaka mkubwa tu na tushamuona hapa akitembelea kaburi la babu, anaitwa J.J (Job), naye tunampongeza kwa kupata dada.

Tunamtakia mdau mpya Mungu amjaalie afya njema na maisha merefu yenye kheri na baraka tele.

Thursday, September 10

Karibu Khloe Mfumu



Nachukua nafasi hii kumkaribisha mdau, Khloe Mfumu, ingawa si mdau mpya, maana alikuwepo tangu enzi za kijuficha kwa mama.
Amezaliwa tarehe 09, mwezi wa 09, mwaka wa elfu mbili na 09, saa tatu usiku, tukiandika kwa kudhungu si ndio inakua 09, mi naomba nimwite tisa tisa, maana hii nimeipenda.
Baba mtu, Innocent Mfumu anasema wakati kwa watanzania woote kitu cha muhimu na tulichokuwa tunakikodolea macho saa hiyo ilikua hotuba ya kipekee ya JK, yeye alikua anakodolea macho kitu muhimu kuliko vyote kwake, Khloe.
Hongera mama, Rosemary wa HIMA Tours.

Friday, August 7

Karibu Ashlyn

Wadau wa mama na mwana tunamkaribisha mdau mpya, Ashlyn Kerya, aliyezaliwa wiki iliyopita, tarehe 31, July. Tunawapongeza mama, Goodlove Lwayu na baba Albinus Kerya kwa kupata mtoto mzuri wa kike.
Mungu awabariki.

Thursday, May 28

Breaking Newzzz...Mdau Mpya toka kwa Hilda na Benja

Bado niko kwenye mshtuko wa furaha baada ya kupata taarifa sasa hivi toka kwa Benjamin Mwanambuu, kuwa kipenzi chake, Hilda Chuma amejifungua mtoto wa kiume dakika chache zilizopita.
Mungu awabariki sana rafiki zangu hawa wapenzi kwa kutuletea ingizo jipya na kukamilisha furaha yao.
Kwa niaba ya wadau wooote wa Mama na Mwana hongera sana mama, Mungu akubariki wewe na mwanao muendelee kuwa na afya njema.
Jamani nina furaha sana, hata natamani nitoke sasa hivi kumuona huyo mtoto.
BTW: Pix coming soooon.

Friday, March 13

Breaking Newzzz...Zeze Katuletea Fashonista

Nimepata habari sasa hivi, kupitiakwenye comment ya mdau Mama Raheem, kuwa Shostiso Sahmimu Zeze wa 8020 Fashions amejifungua mtoto wa kike usiku wa kuamkia leo.
Kwa niaba ya wadau wooote wa mama na mwana hongera sana mama, Mungu akubariki wewe na mwanao muendelee kuwa na afya njema.
By the way, huyo mchumba alishawahiwa na X tangu akiwa tumboni!