Thursday, September 10

Karibu Khloe Mfumu



Nachukua nafasi hii kumkaribisha mdau, Khloe Mfumu, ingawa si mdau mpya, maana alikuwepo tangu enzi za kijuficha kwa mama.
Amezaliwa tarehe 09, mwezi wa 09, mwaka wa elfu mbili na 09, saa tatu usiku, tukiandika kwa kudhungu si ndio inakua 09, mi naomba nimwite tisa tisa, maana hii nimeipenda.
Baba mtu, Innocent Mfumu anasema wakati kwa watanzania woote kitu cha muhimu na tulichokuwa tunakikodolea macho saa hiyo ilikua hotuba ya kipekee ya JK, yeye alikua anakodolea macho kitu muhimu kuliko vyote kwake, Khloe.
Hongera mama, Rosemary wa HIMA Tours.

2 comments:

Anonymous said...

hongeleni sana wazazi ni kabinti kazuri kweli mmepata. namtakia kila la heri na baraka nyingi katika maisha yake yanayomsubili mbele.

Anonymous said...

Hongera sana Inno. Umekuwa sasa, ila mbona umetuharibia mchumba huyo. Ona alivyochukua pua yako.
Mungu awabariki sana na mumlee vyema. Ila jina hilo jamani Mh! Bibi na babu yake sijui kam wataweza kulitamka au ndo itabaku kuitwa K tu.