Thursday, May 28

Breaking Newzzz...Mdau Mpya toka kwa Hilda na Benja

Bado niko kwenye mshtuko wa furaha baada ya kupata taarifa sasa hivi toka kwa Benjamin Mwanambuu, kuwa kipenzi chake, Hilda Chuma amejifungua mtoto wa kiume dakika chache zilizopita.
Mungu awabariki sana rafiki zangu hawa wapenzi kwa kutuletea ingizo jipya na kukamilisha furaha yao.
Kwa niaba ya wadau wooote wa Mama na Mwana hongera sana mama, Mungu akubariki wewe na mwanao muendelee kuwa na afya njema.
Jamani nina furaha sana, hata natamani nitoke sasa hivi kumuona huyo mtoto.
BTW: Pix coming soooon.

2 comments:

lucky said...

woow!!! jamani hongera sana dada yangu. hata mi natamani kuja kumuona mtoto. nimekukumbuka tangu enzi zile za bwiru girls. hongera sana mpendwa na mungu awajaalie afya njema na maisha ya furaha.

Anonymous said...

Hilda hongera Mungu awatunze wewe na mwanao tulisoma wote bwiru girls tho nilikuwa nimekutangulia kidato kimoja ila nakukumbuka vizuri i wish ningekuona tushare furaha BE BLESSED
RUTH KIRANGI
EX- BWIRU GIRLS