Showing posts with label Day One. Show all posts
Showing posts with label Day One. Show all posts

Tuesday, August 13

Karibu Suzan



Mdau mpya ameingia mjini,anaitwa Suzan hapa akiwa na siku nne duniani.nampenda sana baby suzan namtakia maisha marefu.
Mama Suzan.

***
Mama na Mwana inakukaribisha duniani na kwenye playground yetu hii hapa Suzan.

Thursday, March 8

Mdau mpya - Emmanuel




Emmanuel: Kwa wakristo maana yake ni Mungu pamoja nasi.
Alizaliwa Dec 4, 2011.

 Emmanuel ( he is very handsome) na ma'mtu wakipozi. Pole kwa ma'mtu alijifungua kwa C-section.


Like mother like son.

 Waki show love na Cleopatra.( Dada na kaka).

  Mama ya Cleopatra na mama ya Emmanuel ni mtu na mdogoye.

 Mama ya Emmanuel akiwa kwenye safari ya mwisho ya kumngoja mgeni.


 Cleopatra nae hakuwa nyuma kumngoja mdogo wake kwa hamu kubwa sana.

Kila la heri mama Emma katika makuzi ya mtoto.

Wednesday, February 29

X ingizo jipya!

New family member anaitwa Xyleen Lerato Mapunda...hii ni few minutes after birth!
During my time out nimeleta kitu kipya! Huyu ni mdogo wake Xchyler, anaitwa Xyleen (tamka Shyleen) kifupi ni Xy (Shy). So unaweza kuniita 'Mama X squared'.

Kaka mtu, aka Biggie aka X anampendaaaaaa balaaa...! I know for sure anampenda kuliko mtu yeyote!


X alikuwepo tangu mwanzo, alikua anamsubiri kwa hamu huyo mtoto...


Safari yake ilianzia wakati uleeeee nikiwa SA, so ndio maana tukampa jina la kati  la Lerato lenye sili ya ki-Tswana lenye maana ya pendo.
...Pozi la tumbo....



Bize hadi siku ya mwisho...
 Hii ilikua kama siku tatu before kumpokea mgeni huyo...nilienda kazini hadi Ijumaa, Jumamosi mchana nikaenda hospitali, nikajifungua usiku wa kuamkia Jumatatu.





Binti shashiriki matukio mengi ya kifamilia, ikiwamo hii graduu ya dady...
 Kuna walionitumia msg kuuliza kama huyo hapo ni X, yes, ni yeye akiwa na memba mpya wa familia, wakimpa tafu dady kwenye mahafali. (Huyo ni classmate wa dady, Hoyce Temu).




anapenda sana kucheka.

Leo anatimiza miezi sita ya kuzaliwa, so alizaliwa August 29, 2011. Ana kajino kamoja, hiyo picha ya kajino bado sijaipata, maana ni la chini, so kulipata kwenye pozi si kazi ndogo! Katika miezi sita hii kuna mengi ya kusema juu yake, ila mtamjua tu taratibuuu...


...na hapa kwenye bembea yake humtoi!

Of all the things anapenda kula, anything, ila haswa nyonyo!!!
hapa na dady home...

Nashkuru Mungu nimepata shost wa ukweliiii...swali ni nimejizaa au sijajizaa???

Mdau na wewe una update? Iwe la mdau huyo huyo wa zamani tunayemjua au una ingizo jipya we tuma kwenye mamanamwana@gmail.com, maana nimewamisi wadau wangu balaaa!

Thursday, May 20

Karibu Jenipher

Mama na Mwana kwa niaba ya wadau wooote tunafuraha ya kumkaribisha mdau mpya aliyezaliwa tarehe 5, May mwaka huu, pale hospitali ya Bugando, Mwanza.

Wazazi wake wana .furaha kubwa kwa ingizo hili jipya la furaha kwenye maisha yao. Mdau amepewa jina la Jenipher. Picha hizo juu mbili ni muda mchache, kama dakika tano tu, baada ya kuzaliwa.

Mdau pia ana kaka anayeitwa John, kwa hiyo mama yao, Emmy siku hizi unaweza kumwita Mama J's. Naona baada ya kuulizia watoto no 2, napewa majibu ya vitendo, si maneno, kumbe wadau walikua njiani.
Hapa ni siku ya pili baada ya kuzaliwa...beautiful...Mungu amjaalie mdau na mama mtu afya njema na maisha yenye kheri na baraka tele.

Friday, March 19

Karibu Fahim

Mdau mpya, anaitwa Fahim Fadhili, amezaliwa Jumanne iliyopita, tarehe 9 March.
Ba'mtu Fadhili Akida ana furaha isiyo kifani.
Hongera baba na mama kwa mtoto wa kwanza.

Sweeeeet!
Mama na Mwana tunamwombea Mwenyezi Mungu ambariki mdau mpya maisha mema yenye afya na kheri tele!

Monday, February 15

Karibu Elizabeth Valentine

*Valentine baby*
Anaitwa Elizabeth Valentine (mi ntamwita Liz V), amezaliwa jana alasiri, hospitali ya Agha Khan. Hii picha ni ya leo asubuhi, keshachangamka!

Mama na Mwana inawapongeza Jacqueline na Aaron Suluba kwa ingizo jipya. Huyu ni baby No Two, ana kaka mkubwa tu na tushamuona hapa akitembelea kaburi la babu, anaitwa J.J (Job), naye tunampongeza kwa kupata dada.

Tunamtakia mdau mpya Mungu amjaalie afya njema na maisha merefu yenye kheri na baraka tele.

Sunday, December 6

Warren

Mdau mpya Warren S. (si unaona kadi hapo juu inaonyesha, wameweka na kiganja na unyayo wake...sijui nchi gani hii). Amezaliwa tarehe 10 Oct 2009, hapa alivyotoka kuzaliwa tu, soooo cuuuute!

Cuteee....

Mam'tu katoka bomba...na hiyo stroller imempendezaaa.


Cute, cute, cute.

Tuesday, November 17

Prescious Prescious...

Mimi naitwa Precious Anthony wa Dar es salaam.
Nina Umri wa miezi miwili sasa, ningependa kubadilishana mawazo na wadau wa hii blog. Hii picha ni siku nipoingia ulimwenguni, nitazituma nyingine zaidi baadaye.
Asante. Nawakilisha.
Precious.
*****
Na sisi tunakuambia karibu sana Prescious, hii picha inanifanya nitamani mtoto mchanga...sooo beautiful.

Friday, February 6

Introducing Harriet

At last baada ya kumtembelea hivi karibuni nimefanikiwa kupata picha za mtoto wa modo wetu, Regina Kumba, anayeitwa Harriet aliyezaliwa tarehe 9 Jaunary. She is such an angle.

Saturday, December 27

Triplets for X Mas

Bi Mariam Rajabu Mkazi wa Mwanayamala A Dar es Salaam, amejaaliwa zawadi tatu krismas hii. Mariam amejifungua mapacha wa tatu katika Hospitali ya Mwananyamala na yupo katika mtihani mzito wa juu ya kuwalea watoto hao watatu ambao mmoja kati yao ni wa kike.Kwa mujibu wa Mariam anasema aliyempa ujaziuzito huo alimkana tangu mwanzo na hamjali kwa lolote na Familia anayoishi nayo pia ni maskini. Na tangu amelazwa hapo hakuna yeyote aliyefika kumjulia hali na anategemea msaada mkubwa wa wauguzi. Anaomba yeyote aliye na msaada wa hali na mali chakula au mavazi asisite mkusaidia ili kumpunguzia ugumu wa kulea viumbe hivyo visivyo na hatia vilivyozaliwa katika kumbukumbu ya kuzaliwa Kristo Yesu au Nabii Isa.
Yeyote mwenye msaada awasiliane na Mroki Mroki wa http://www.mrokim.blogspot.com

Thursday, December 11

Kelvin - Day One


Kelvin Pongo mtoto wa Thecla mara baada ya kuzaliwa siku ya tarehe 11 April 2008, Muhimbili Hospital.

Friday, November 28

Jay - Day One

Sweet Baby, Jayson James baada ya kuzaliwa siku ya Jumatano, tarehe 14, May, 2008, Agha Khan Hospital. Mama yake ni Jacquline Sadicky.

Tuesday, November 25

Dalvis - Day One

Dalvis Mlingi, mtoto wa Joyce Macha mara baada ya kuzaliwa siku ya tarehe 24 January 2008, Agha Khan Hospital.

Monday, November 17

Xchyler - Day One

Xchyler wangu mchana wa tarehe 16 April 2008, alizaliwa usiku wake. Nakumbuka siku hiyo, alikua mpole,mtulivu, yani alikua mtoto kweli, sasa hivi ni fujo tu!
  • Unakaribishwa kutuma picha za siku ya kwanza ya mtoto wako.
  • Kuona za wengine bofya hapo kwenye Day One.
  • Kusoma kuhusu watoto waliozaliwa karibuni bofya Birth.