Aisee siku moja nilimtembelea rafiki yangu, tulikuwa wageni kama wanne hivi tofauti. Pia alitembelewa na ndugu yake mwingine akiwa na mwanae wa kiume mwenye umri kama miaka saba hivi.
Aisee yule mdau alikuwa mtata balaa. Alikuwa anaongea sana tena hovyo na matusi mdomoni bila kujali anaongea na nani. Wakati tuko kwenye pilikapilika za hapa na pale bahati mbaya mgeni mwingine tuliyekuwa naye akakanyagwa.
Akamuuliza jamani mbona umenikanyaga? Jibu lililotoka hapo "Aaah nini bwana we, mi mwenyewe umeniumiza na makucha yako". Mungu wangu mama yake alikuwepo ila hakusema kitu chochote zaidi ya kuona aibu na kunung'unika.
Hiyo ni Intro zama ndani ujue kilichojiri zaidi
Kwanza yule mdau hakupenda kabisa kukaa na watoto wenzake. Akicheza nao dakika tano tu tayari ni kesi tu na mashtaka ya kutukanwa yanaletwa tulipokuwa tumekaa. Sasa akawa anakaa watu wazima walipo wanachoongea na yeye anaingilia na kuleta stori zake za makorokocho.
Yani sasa baadaye wale wakubwa walikuwa wananyamaza wanamuacha mtoto anaongeaaa kama dakika 5 kisha akinyamaza maongezi yanaendelea. Yani ilikuwa ni aibu na sikupenda ku imagine siku mwanangu akiwa vile. Akifukuzwa alikuwa haondoki. Mama yake kwa aibu hakuweza kuthubutu kukaa pale akaenda kukaa pengine na watu wengine.
Tulipopungua baadaye, nilipata wasaa wa kuzungumza na yule mama ndo kutuhadithia sasa. Kwamba yule mtoto hata aseme nini hawezi kumwogopa kwa kuwa baba yake alishamwaribu. Hata mama akimchapa fimbo moja baba akirudi akipata taarifa atatoa mvua ya matusi ikiwezekana na kipigo juu tena mbele ya mtoto.
Nilimuonea huruma sana yule dada lakini pia nisijue kitu cha kufanya kumsaidia.
Baadaye tuliachana kila mmoja akarudi kwake ingawa ile picha ya yule mtoto haitaki kabisa kufutika akilini.
Wapendwa tujadili kama hili linakutokea kama mzazi itabidi tufanye nini? Tujadili wapendwa.
5 comments:
mama x mungu ana mitihani yake ya maisha na huo ni mtihani tena wa darasa la saba, sipati picha mtoto kama huyo unaanzia wapi, nitajaribu maoni yangu mwenyewe sijui hata hiyo tabia unaanza kuikaripia wapi, nionavyo mimi mama mtoto hajasimama kidete katika kuongoza mtoto alelewe vipi, kwa maana angemuwekea mtoto sheria wakubwa wakiongea usiingilie na kama una swali unakuja kunikonyeza sikioni kwa taratibu mama naomba nikuulize, pili mtoto akichokoza wenzake na wenzake wakija shitaki amwambie kosa lake umemtukana mwenzako ni vibaya muombe msamaha tena unamkomalia amshike na mkono akiomba msamaha hiyo itamfanya mtoto kwanza aone aibu na kujirudi kidogo. kuhusu tabia ya baba yake hapo ndipo matatizo ya mtoto yalipoanzia ningemkomalia baba acha kunitukana mbele ya mtoto, na mtoto ukimuonyesha kuwa mimi sio mtu wa kumuadhibu hawezi kunisikiliza na kama baba hasikii ningeongea na wazee wamkanye hiyo tabia ya kutukana mama mbele ya mtoto. haya nimejitahidi nawaachia na wadau wenzangu nao watoe ya kwao tusaidiane ulezi
Tatizo wazazi wengi (hasa sisi wanawake) ukiacha huyo mwanaume, wanashindwa kutofautisha KUMPENDA mtoto na KUMDEKEZA (KUMHARIBU). Unakuta mtoto anamwogopa mtoto kumwadhibu au kumrudi akiwa na umri wa mwaka mmoja, sasa unatarajia akifikisha miaka mitano na kuendelea si atakuwa kidume cha nyumba? Katika malezi ni pamoja na kuhakikisha mtoto anawajibika kwa vishughuli vidogovidogo ndani ya nyumba. Kwa mfano mtoto unamwanzia kwa kumwambia akimaliza kula chakula, aondoe sahani ampelekee dada jikoni na si kumaliza kula anaondoka na kuacha sahani. Yapo mambo mengi baadhi ya wazazi wanawalea watoto wao kimayai mayai lakini hasara zinakuja baadaye anapokuwa ameshindikana kama huyo mtoto.
nafikiri kuna pengo au kitu kikubwa sana kati ya baba vs mama-hapo ndo tatizo na likishughulikiwa ilo lao kwanza then lafata la kumwelimisha mtoto kwa adabu na kumkanya kila afanyapo kosa
NARUDIA: kwanza baba vs mama wapatane kwa lolote walilokosana adi uyo baba kumtwanga na kumtukana mkewe mbele ya mwanae mana ilo ndo mtoto analotilia kibuli,wakipatana hapo kumkanya mtoto ni jambo dogo sana tu
Nakubaliana na anyony wa tatu...tatizo loko kwa wazazi, wakiweka mambo yao sawa ndipo watakapoweza kulea mtoto...kwenye malezi ya mtoto wazazi mnatakiwa muwe kitu kimoja, mtoto akishaona division tu anaitumia kwa advantage yake na ni rahisi kumpoteza...very sad kusikia mtoto asiye na adabu afu amam anaona hana cha kufanya!
Nakubaliana na anyony wa tatu...tatizo loko kwa wazazi, wakiweka mambo yao sawa ndipo watakapoweza kulea mtoto...kwenye malezi ya mtoto wazazi mnatakiwa muwe kitu kimoja, mtoto akishaona division tu anaitumia kwa advantage yake na ni rahisi kumpoteza...very sad kusikia mtoto asiye na adabu afu amam anaona hana cha kufanya!
Post a Comment