Wednesday, December 17

Baby Milestones

Tabasamu

Hapa X akitabasamu kwa mbaaali bila kujijua, the next minute akatoa kilio. Hapo ana siku kama 28-30 hivi.Hii ni moja ya tabasamu zake za mwanzo kabisa. Alivyomaster hiyo skill, kama sasa hivi, akikuangalia halafu akakupenda anakupa bonge la smile, si ashagutukia kuwa ni ishara ya upendo.

Hamna kitu kitamu kama mwanao akikuangalia halafu akatabasam, yani akusmilie, unajua nini kuhusu mtoto kutabasamu?
Smiling, kutabasamu, ni hatua ya kwanza ya mtoto katika kutaka kujichanganya na watu. Ukiona mwanao anaanza kutabasamu ujue ameshaanza kuelewa jinsi ya kuhusiana na anaanza kutofautisha furaha na huzuni.
Tabasamu ya ukweli huwa inaanza mtoto akiwa na miezi mitatu, ambapo anaitumia kama inavyotakiwa, kuonyesha furaha na mapenzi,. Kabla ya hapo (mara nyingi kuanzia mwisho wa mwezi wa kwanza) huwa anaitoa tu bila kujua kazi yake na wala haicontrol, yani inajijia tu.

No comments: