Tuesday, December 2

Maandalizi ya Mtoto


Cheki Gladys Fahari alivyometisha blanket na kishati cha mwanae Mwita, isnt he cuuute? Subiri tuone mtoto wa pili atavyochanganyiwa rangi kama kachumbari.

Mtoto wa Kwanza: Unafua nguo zake zote, unazinyoosha zote unazikunja vizuri na kuzipanga kwa kumetisha rangi kabatini.
Mtoto wa Pili: Unaziangalia tu zile nguo za mototo wa kwanza kama safi, au kama vipi unazifua na kuzipanga.
Mototo wa Tatu: Wavulana wanavaa tu hata pink! Anything goes.

5 comments:

Anonymous said...

ila kweli jamani, watoto wa kwanza huwa wanachangamkiwa sana, hata na ndugu, marafiki na jamaa. sasa sisi wa katikati ndio huwa tunasahaulika kabisaaa, afadhali hata wa mwisho kidogo.

Anonymous said...

Huuu ni ukweli kabisa. mtoto wa kwanza unakuwa so excited. Wakati mwingine nikifikiria najioni I was over working myself. But it pays, that is the price of parenthood.

Anonymous said...

Mtoto wa kwanza ana jinsi yake ya pekee, siwezi kuexplain ila napenda wanangu wote.

Anonymous said...

ah umenichekesha sana, hasa muhusu mtoto wa tatu kuchanganyiwa rangi hata pink kwa mtoto wa kiume. Mi nna mtoto mmoja,nampenda sana, na shughuli ni nyingi kama ulivosema maybe kwa sababu ni wa kwanza lakini naomba Mungu nitakapojaliwa mtoto mwingine nisibadilike, yani nimjali kama dadake, unajua hii tofauti katika kuwa treat watoto ina waathiri kisaikolojia badae wakikua, wanajiona kama hawana thamani.
ntakutumia picha ya Frida soon. love ua blog,
mama Frida,NL

Anonymous said...

Hi dada,
mimi nina mtoto mmoja tu ana miezi 4, yani attention yote kwake i take my time hata kama ni lisaa moja kumchagulia nguo, anamatch kila kitu mpaka soksi mpaka bibo yake hata akiwa ndani achilia nikitoka nae labda kwenda clinic ndo usiseme. nakapenda sana katoto kangu jamani, full attention kwake. naomba na mtoto wa pili nae iwe ivi ivi.
mama P