Monday, January 26

Mdahalo: Mtoto wa Kisahili Haendi Bila Fimbo

Enzi zetu tulikuwa tunachapwa shule ile mbaya, hata kwa kosa dogo tu lisilo na maana, mwalimu anashika fimbo kibano. Siku hizi mambo ni tofauti, hizo academy hazina muda wala hazioni umuhimu wa kuchapa mtoto.
Na haikuwa shule tu, wazazi wa enzi hizo walikua na fimbo maalum ya kuchapia watoto ndani, kama hamna ukifanya kosa inaende kuchumwa, au wengine ni mkanda tu utatumika. Ila siku hizi, wazazi hata kugomba hawajui, nini kuchapa.
Lakini kuna wanaosema kuwa mtoto wa Kiswahili haendi bila fimbo, so tabia ya wazazi na waalimu wa siku hizi inasababisha mmomonyoko wa maadili, wadau mnasamaje?

2 comments:

Anonymous said...

Wazazi wa enzi hizo waliamini katika ubabe si kwa watoto hata wanaume walikuwa wakitumia mikwaju kuwaweka sawa wake zao.

Kizazi cha sasa ni cha dot com, kwanza watoto toka wanazaliwa ni wababe na wabishi, watoto wa kike ndo usisema mzazi akileta longolongo hawachelewi kujidunga sumu.

Kwa nini wazazi hawachapi watoto hivi sasa: bakora sio njia muafaka ya kurekebisha tabia ya mtoto, ni hatua ya mwisho baada ya mtoto kushindwa kufuata maelekezo sahihi ya mzazi/mlezi tofauti na zamani ambapo wazazi walitumia bakora kama njia ya kutisha.

Mchape ovyo mtoto wa sasa uone shughuli yake kama hujapigwa ngumi, mawe basi tarajia mvua ya matusi.