Monday, March 23

Lishe ya Mtoto Baada ya Maziwa - Kuanza


Lishe After Maziwa
Wadau mbalimbali wamekua wakinitumia mails kuniulizia kila kitu kinachohusu kulisha mtoto chakula, kuanzai jinsi ya kumuanzisha, lini aanzishwe hadi apewe nini.
Kiukweli nimejitahidi kujibu, sasa naona zinanielemea na wadau mtaona siwajibu labda nimewachunia, ila si hivyo, na ili kuondoa tatizo hili wiki hii nzima ntapost maelezo yoote kuhusu kumuanzisha mtot vyakula zaidi ya maziwa, wadhungu wanaita solid foods, kwetu ni vitu kama uji.
Vitu nnavyoweka nimetoa kwenye websites mbalimbali, na kuvitafsiri na kuboresha, ila ili kuwa realist zaidi chini ya kila posting ntakuwa naweka Xchyler’s Experience, ili niweze kuelezea ninavyofanya mimi mwenyewe kwa mwanagu.
Pia mtu ataweza kuzipata postings ambazo labda kwa bahati mbaya zimampita kwa kubonyeza label ya Lishe hapo kushoto, ambapo atapata zooote zilizitoka.
Pia wadau, ntahitaji picha za watoto wakiwa kwenye msosi, hata kama wachafu, au dada anamlisha, au unamlisha wewe na wote mmejaa uji hadi kichwani, ili niwe naziambatanisha, leo naanza na Big X mwenyewe.

Lini Uanze Kumlisha Mtoto Vyakula Vingine?

Wataalam wa lishe ya watoto wanasisitiza kuwa Ni muhimu kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee mara anapozaliwa hadi anapotimiza umri wa miezi sita. Hii ina maana kwamba mtoto asipewe maziwa mengine yoyote, vyakula au vinywaji ikiwa ni pamoja na maji.
Hata hivyo wataalam wengi pia wanashauri uanze kumpa mwanao vyakula vingine, zaidi ya maziwa, kuanzia miezi mine (4) hadi sita(6). Baada ya miezi 6 maziwa ya mama pekee hayatoshelezi mahitaji ya mtoto. Hivyo mtoto aanze kulishwa taratibu vyakula vya aina mbalimbali ili aweze kukua vizuri.

Xchyler’s Experience
X alianza kula vyakula vingine akiwa na miezi mitatu kamili, as nilijua ntaanza kwenda kazini wiki mbili zilizofuata, na mimi sikutaka kabisa mwanangu anywe fomulasr, au kitu chochote cha kwenye makopo, na sikutaka anywe maziwa ya ng’ombe hadi afikie miezi sita, so nikaanza na uji.
Kabla ya hapo alikua anakunywa maziwa yangu tu, hata maji alikua hanywi, na uzuri mama yake na uslim wangu maziwa yalikua yanamshinda mwenyewe kwa jinsi yalivyokua mengi.

NB: Jitayarishe na vifaa maalum vya mtoto, X ana visufuria vyake, vibakuli yake, chupa zake, kila kitu chake, yani Bibi akikukuta unampikia mjukuu wake kwenye sufuria nyingine ugomvi mkubwa.
Kifaa nilichokipenda kuliko vyote, vijiko soft vya plastic vya watoto, maana katika kulishana ukitumia kijiko cha chuma unaweza kumuumiza fizi, afu akapata kidonda akawa anakataa kula usijue kwa nini. Nilinunua seti spesheli ilikua vinauzwa kuna vibakuli, vikombe, vijiko huko Game section ya watoto, sijui kama bado vipo.

2 comments:

Anonymous said...

hapa ni kasheshe, mpaka visufuria vyake??? vibakuli, kikombe, vijiko ofcourse ila visufuria hapa ndio usipoangalia mahousegirl wanatimua, hapa tuangalie hili nalo mama X

MAMA MAY said...

kwa kweli nimependa sana ulivyofafanua kuhusu vitu vya mtoto. NI muhimu sana awe na vitu vyake mwenyewe tena hata katika kuvihifadhi VIHIFANDHIWE SEHEMU YAKE MWENYEWE VIWE VIMEFUTWA KABISA NA KITAULO CHAKE BINAFSI KIZURI NA KISAFI. je ni sasa mtoto wa miezi 4 kunywa uji mara 3 na maziwa mills: 150 mara 2 kwa siku? mama yake anaenda kazini saa 4 ikiwa amemnyonyesha anarudi nyumbani saa 1 usiku ndipo ananyonya tena. pls wadau. kwa mwenye ushauri au maoni.