Monday, March 23

Xchyler Anaogelea

Wikendi ilee, ya tarehe 15, Xchyler alialikwa na mdau Aurelia kwenda kuogelea kwao. Kama anavyoonekana kwenye hizi picha ingawa ni mara ya kwanza kuogelea inaelekea mwanangu ana kipaji cha kuogelea, au wazungu wanasema 'he is a natural' hana wasiwasi. Na expert swimmer, Aurelia Croft (miaka 2) alikua anaonyesha mfano, maana yeye alianza kuogelea wiki chache tu baada ya kuzaliwa.
Hapa anasikilizia utam wa maji.


Hapa anatest akisimama maji yatamfikia wapi, hana wasiwasi!


Hapa anaelea elea flan hivi.

Huyu ndio expert swimmer, Aurelia akichekelea maji.

Aurelia anaweza vitu vingi kwenye maji, amesha yazoea, hata kuzamia chinikwa chini anaweza, sasa kasheshe ni kumtoa hapo, huo ugomvi wake, si kidogo, akishaingia huwa hataki kabisa kutoka.

No comments: