Saturday, May 2

Ubatizo wa Big Psalm

Hapa ilikuwa ni siku ya Pasaka, ambapo Big Psalm alibatizwa rasmi na Padri Mapunda wa Kanisa la Anglikana usharika wa Isanga, jijini Mbeya ambapo baada ya ubatizo Psalm akiwa na kundi lukuki la wajukuu wa Mzee Mng'ong'o walikwenda nyumbani kwa ajili ya shughuli za sherehe, anbapo siku hiyo watoto wengine wawili akiwemo wa baba yake mkubwa Big Psalm alibatizwa.

Big Psalm akipiga makofi baada ya kufurahishwa na burudani, hapa kilichomfurahisha ni wimbo wa jipange sawa sawa.
Hapa akijadiliana jambo na mama yake mara baada ya kupiga simu hiyo.
Kumbe alisahau kupiga simu ya muhimu, hapa alikuwa tayari amenyang'anya simu ya baba yake na kuwasiliana na mimi ili kunitaarifu nimwekee nafasi ya picha zake.

Psalm vipi bwana, hapa alikuwa akiendelea na hekahela na kuhakikisha anafungua box la zawadi.
*****
Thanx Baba Psalm for the pix.


No comments: