Wednesday, November 11

Watoto kukataa kula - Janga letu sote

"Hellow mama X vipi mambo. mimi naitwa mama Julius wa Tabata kimanga Dar es salaam. napenda sana kuifungua blog yako kila siku. inatusaidia sana hasa sisi wenye watoto wadogo. masikitiko yangu ni juu ya mwanangu J, kwa kweli hana afya nzuri hata kidogo na wala si mgonjwa. ni mzima kabisa wa afya na kwa sasa ana mwaka mmoja na miezi mitano bado ananyonya, ni mtundu sana na hapendi kula hata umbembeleze vipi hataki chochote. nakata tamaa kwani hata nipike mlo wa aina gani hataki.juice hataki ata iwe yanini maziwa ya ng'ombe ndio kabisa ukimpa anajitapisha. supu ta nyama kidogo anaipenda.navunjikamoyo na roho inaniuma pindi ninapoenda clinic na kukuta watoto wengine wanaafya nzuri na ukiuliza vyakula wanavyokula ni vya kawaida kabisa. sasa sijui nifanye nini. nampenda sana mwanangu kuliko kitu chochote duniani.ananipa mawazo ile mbaya. naomba unishauri nifanye nini juu ya hili tatizo la mwanangu kutopenda kula. please help me."

Jamani wenye watoto wapenda kula msaidieni mdau, na wengine maana sha tumiwa mail nyingine nyingi tu zinaulizia suala hili hili, kwa kweli mi jibu sina, X mambo hayo hayo tu (kujitapisha sijui kaanza wakati ana miezi mitatu)...Janga la kitaifa!

6 comments:

Anonymous said...

mmhhh,siwezi sema kwakweli ni JANGA la kitaifa ,ila mimi dada ndo akimpa anakula vizuri sana,ila nikisema nimpe mimi mamake loooo tutakesha na kilio juu

wangu pia ana mwaka na miezi 5/6 anakula viazi,ndizi,wali {ule bokoboko},ugali ,mchicha ,matembele,nyama kidogo ...yeye supu ni BIG NO,paja la kuku anapenda . mjaribishe hivi vyakula

na pia ukiweza jaribuni kumlisha mazingira tofauti ,sio kila siku hapo hapo au chakula hicho hicho anachoka,au wengine humuweka mtoto kwenye kigoda na kuweka tumaji kidogo ya uvuguvugu kwenye kibeseni ili awe anapigapiga viguu vyake kwenye maji

WISHING YOU ALL THE VERY BEST

JOYCE said...

pole sana mama J kwa mawazo ya mwanao kwa kutokupenda kula, mimi pia nina mtoto mdogo wa mwaka na miezi 3 alikuwa anapenda kula sn lakini tangu ameanza mwezi wa tatu huu yani kabadilika hapendi tena anabana mdomo tu na kutema, ila nashukuru mungu dada yake amemjulia anasema eti yeye anamlisho kidogo kidogo kila wakati sio kingi kwa wakati mmoja,alafu huyo J km anapenda supu ya nyama ndo mkazanie hiyo hata ya kuku wa kienyeji weka na mchicha kidogo na karoti ili apate na vitamini nyingine humo, mlishe kidogo kidogo hata km ni nusu kikombe kila wakati utaona mabadiliko mama J.
MIMI NI MAMA COLLIN FRANCIS WA ARUSHA.

Anonymous said...

Pole dada weye, mimi bado sijazaa ila nitakueleza kile kidogo ninachokijua,watoto mara nyingi akifikia umri fulani hujiona kama kawa mkubwa sawa na nyinyi hivyo basi jaribu kula naye wakati na nyinyi mnakula yaani watu wazima wa familia hiyo, pia kama unakaa karibu na watoto wadogo wengine kama ni wandugu au majirani waite wakati anakula ili afanye kama mashindano,epuka kulisha vyakula vyenye michanganyiko mingi kama unaweka unga wa dagaa,karanga maharage kwenye uji vitu hivi vikichanganywa kunawakati husababisha mtoto akatae kula. Usimpe vyakula vyenye mafuta au harufu kali,na jaribu kupika chakula kama cha mtu mzima kidogo usisage kila kitu hii ni kwa watoto walio wakubwa kidogo. Na kama ni mbishi sana jaribu kumpa chakula wakati ananjaa.Pia jitahidi kuwa mchunguzi anapenda kula nini zaidi nadhani kama akikataa vyakula vyote kuna kimoja atakuwa anajitahidi basi hichohicho mkazanie.Ikishindikana hapo ni maombi yaliobakia kwani watoto hawatabiliki na inauma kumuona mtoto anakondeana kila siku wakati unauwezo wakumlisha chochote.

Anonymous said...

Mama J pole na hekaheka za kukuza kwa ufupi ni kwamba
1.unatakiwa usimlazimishe chakula mtoto saa nyingine wazazi hudhani kung'ang'aniza kumpa chakula mtoto ni kumsaidia hapana hilo ndilo kosa kubwa kama unahisi kijana ana njaa na hataki kula jaribu kumpa chakula hicho hicho baada ya muda kama nusu saa akikataa muache mjaribu tena baada ya nusu saa ingine akikataa muache kabisa na usubiri mlo ujao maana saa nyingine watoto huwa na maringo.
2.Jaribu kumpa mtoto aina mbalimbali za vyakula na jaribu kubadilisha kila siku kama anakataa supu ya ngome jaribu ya kuku kama anakataa maziwa jaribu kitu kingine mdadala ya maziwa kama anakataa juisi mpe matunda kama anakataa kiazi ulaya mpe boga yaani jaribu kufanya uwezalo mwanao awe na kitu mbadala.
3.Usimlisha mtoto wakati hana njaa jitahidi uache masaa kama matano kutoka mlo mmoja kwenda mwingine.
4.Jaribu kumlisha mtoto sehemu yenye ukimya na isiyokuwa na kelele ama vitu ambavyo vitamvutia mtoto asifikirie chakula afikirie hivyo vitu mfano kumlisha mtoto wakati Television inawaka.
5.jitahidi kumpikia mtoto chakula chake mwenyewe epuka kutumia mafuta viungo vikali vyakula vyenye harufu kali, chumvi na mambo kama hayo watoto wengine huwa wapendi harufu fulani za vyakula.
6.Umesema mtoto bado ananyonya sio mbaya jitahidi upunguze kumpa nyoyo huyu mtoto inawezekana tazizo unalileta mmwenye mara baada mtoto akikataa kula unadhani nyoyo itamsaidia so unampa hii inachangia kuharibu mtoto asile mtoto maana anajua nikikataa kula kuna nyoyo so punguza kumpa mtoto nyoyo kwa umri wake anatakiwa kula chakula na nyoyo ni ya kujazia vitamins zinazokosekana.
Kwa kufunga kina mama tuondoe mawazo potofu ya kwamba afya ya mtoto lazima awe na mapingilipingi ndo tuseme mtoto ana afya mtoto kuwa na furaha ,kutoumwa mara kwa mara na kucheza bila matatizo ni afya tosha tusidanganye na mapingilipingi tukidhani ndo afya huku tunawauwa watoto taratibu tukiwalisha wenetu kupita kiasi na kwa mashindano eti aonekane mwenye afya.
Mama Ethan.

Anonymous said...

watu wameongea vizuri hapo juu mimi nilikuwa na tatizo hilo,nafikiri uache kunyonyesha maziwa saa nyingine hataki kula kwani anajua maziwa yapo mie nilimuachisha mwanangu alipofikisha mwaka na miezi minne akaanza kula vizuri lakini alikuwa kam mtoto wako,mjaribishe tu vyakula tofauti tofauti na kama una dada akusaidie wakituona tu wanakuwa wanadeka,Pole sana najua unavyofeel
Mama T

Anonymous said...

Hallo mama J, pole najua unavyojisikia lakini wachangiaji hapo juu wamekupa ushauri mzuri sana, zingatia hayo ila usikate tamaa mpendwa, muombe Mungu ampe hamu ya kula mtoto wako. Hakuna kinachoshindikana na baada ya muda mambo yatakuwa bam bam. mama R