Thursday, December 31

2009 Special: Waliofunga miezi 12

Kufunga mwaka huu, ambao unaishia leo nimeamua kutoa list hizi mbili.
Hii ni kwa wale wadau waliofunga miezi 12, yaani wametimiza mwaka mmoja mwaka huu, na kutufanya kuacha kuhesabu miezi tunapotaja umri wao.
Tumesharehekea wote kutimiza kwao mwaka mmoja hapahapa na nawashukuru woooote kwa hilo.

Nawapenda wote, na nawatakia wote maisha mema, yenye kheri na fanaka tele.
Mungu awape wazazi wenu nguvu, hekima, akili, uwezo, maarifa, upendo, hali na mali za kuwawezasha kuwakuza ili mzidi kusherehekea siku za kuzaliwa nyingi mbeleni!

NB: Kama kuna niliyemsahau kwa bahati mbaya wala asijisikie vibaya, anishtue tu, nami nitamjumuisha na wenzake.
Pia nasikitika kwamba sitaweka zaidi ya mwaka mmoja, maana list itakua ndefu sana, na kazi itakua si ndogo, pia naamini kutimiza mwaka mmoja ni hatua kubwa sana kwa wazazi na mtoto, hivyo ndio maana nimeamua kuitambau kwa mwaka huu na mingine ijayo.

2 comments:

Anonymous said...

Haya Jiang mwanangu naona hata nikikutumia picha humuweki nilikutumia picha zake za birthday hukuziweka mpaka kesho anyway tunamuomba X MSAMAHA TULICHELEWESHA KADI ili aje kula keki by the way ETHAN KAARE JUNIOR UMESAHAU KWENYE LIST ALIFUNGA MWAKA NOV 2 2009 TUNAMSHUKURU MUNGU KWA HATUA HII KUBWA MAMA NA BABA ETHAN

Jiang said...

samahani sana mama na baba Ethan, sio dhamira yangu hata siku moja kutotoa picha za mtoto yeyote, hata sijui za mdau Ethan zilinipitia vipi, na kwa sababu hii list niliitoa kwenye zile birthday ndio maana na hapa nikamkosa tena.
Samahani sana kwa hilo, ila nimesharekebisha na sasa yuko kwenye list...juu kabisa.