Monday, January 18

B'day party ya Harieth ilinoga Kigoma

Birthday girl, Harieth Mpogolo, siku ya birthday yake ya kutimiza mwaka mmoja, 7 January, mwaka huu(Samahani nilimpongeza tarehe 9, mtu aliyeniambia habari ya kuzaliwa mwaka jana aliniambia hivyo). Hili ndio pigo lake rasmi la siku hiyo.
Sherehe ilipelekwa Ujiji, Kigoma, kwa bibi mzaa mama, ambaye aliandaa kila kitu, mdau alitua mwisho wa reli siku moja kabla.

...gauni zuri, ila mi nimezimia hivyo viatu, vina urembo hadi kwenye soli, kiua chekundu juu na viua vingine chini...hapa analicheck gauni jipya!

Hii ndio iliyokua tam-tam yenyewe...

Tam-tam inapigiwa saluti...

Harieth hakutaka kukatiwa na mtu, 'wasije wakakata jina bure' keki aliikata mwenyewe...kama aliweza viiile...

1 comment:

Anonymous said...

Nguo mpya raha jamani.
Nakumbuka wifi yangu Mama Rachel alikuwa akienda dukani kununua nguo za kina Rachel lazima awe na pesa ya ziada ya kununua nguo nyingine. Hii ni sababu Rachel alikuwa akipima nguo hataki kuivua ni ugomvi, hivyo inabidi apime za sikukuu then inanunuliwa nyingine simple ndiyo anaondoka kavaa.

kweli mamy kafurahia nguo mpya!!! ukitaka ugomvi mvue

disminder