Tuesday, January 19

Dada mpya!

Baada ya kutafuta kwa takribani wiki mbili, at last nimepata dada mpya mchana wa leo!
Kidogo niugue kichaa, maana sijawahi kukosa dada kwa muda mrefu hivi, ingawa X alikua kwa bibi, wikend alikua kwangu, cha moto nimekiona!
Dada aliyeondoka alikuja Septemba, Disemba ananiambia anataka akale sikukuu ya mwaka mpya kwao, jamani hata hajakaa, ndio kwanza anaanza kujua A-B-C, za kazi, maana hata waajiriwa wa maofisini likizo ni baada ya mwaka, yeye anataka baada ya miezi mitatu, nilichoka!
So aliondoka tarehe 29, ila dada wa kwanza kabisa alikua yupo wakati wa likizo(aliondokaga baada ya kupata shule), nikawa naendelea kutafuta huku huyo yupo.
Sijui kama kuna kitu adimu sasa hivi kama wafanyakazi wa ndani, ndio maana mi nilishaitaga janga la kitaifa, ingawa kuna waliobisha, lakini mi nabaki na jina hilo hilo, wafanyakazi wa ndani ni janga la kitaifa!
Kuwapata kazi, ukiwapata mapozi kibao, ila tunayavumilia, akiona unambembeleza ndio huyo anaaga, he!
Kwa kweli tunahitaji suluhisho la kudumu, la sivyo tutafukuzwa kazi, tubaki nyumbani tunalea watoto tu!

14 comments:

Anonymous said...

Aise mama X ni janga la kitaifa kweli nimepata tabu kupata msichana sisemi ni so, mi nadhani mabinti wengi wanaenda shule baada ya shule za kata kuongezeka ni kitu kizuri ila tunachangamoto ya kulea watoto.

Mama Kelvin said...

Kweli ni janga la Taifa, nami nimepata msichana kwa shida sana alafu ukimpata kununa kwa sana akikosea hataki kuambiwa, unampa simu kwa ajili ya sisi wenye watoto wadogo tuwasiliane anafanya yakutafutia kazi kwingine yaani kuna wakati natamani kumpeleka Kelvin wangu shule mapema ili nisiangaike na wasichana, mimi huwa nawaita wasichana wa kazi ni ugongwa wa moyo.

Anonymous said...

JANGA LA KITAIFA.
Na utadhani wote wameambizana.
% kubwa sana lazima atabadilika.
tena sikwambii sisi tunaowapenda kama ndugu zetu, ndiyo wanatutesa hasaaaaaaaaaaaa.

Angalia kwa wahindi wanavyodumu, na wengine hurudi kubembeleza.
Angalia wale wanaowapiga na kuwatesa wala hawaondoki.
LAKINI WEWE UNAYEMJALI KAMA MDOGO WAKO. LOOOOOOOOOOH

INAUMA SANA, KWANI MTU ANAYEISHI NA MWANAO VIZURI, LAZIMA UMPENDE, LAKINI HAWA WENZETU HATA HAWAPENDEK
TUFANYE NINI?

disminder

Lulu said...

Mweee mi ndo sisemi yaani hili ni Janga kwa kweli, maana kwa mwaka mmoja nimekaa na wasichana zaidi ya sita. Unajua inabidi niwe na wasichana wawili ili mmoja awe wa watoto na mwingine wa kazi za ndani za kawaida lakini ndo du kichefuchefu, unarudi jioni unakuta mambo hovyo kabisa, ila uliza sinama gani hawajaangalia DSTV kila kipindi wanakijua. Sikilizia sasa vitu vinavyopotea humo ndani kila wanapotaka kwenda off, maana nilichukua wa kwa agents duuh!!! Ukiagiza kijijini labda aje ambaye hajasoma, maana waliomaliza darasa la saba wanafaulu wote kwenda kwenye shule za kata. Jamani kama kuna mtu anajua wapi naweza kupata haouse girl wa kulea watoto tafdhali niambie maana kwa sasa nimeazimwa na mama msichana wake. Bora Jiang ambaye mama yake yupo free kukaa na mjukuu, mi mama yangu ni mabusiness na yeye, hana muda kabisaaaaa naye akimtaka mjukuu basi mpeleke na dada yake.

Anonymous said...

nAKUJA DAR KUANZISHA DAY CARE NITAPOKEA WATOTO KUANZIA MIEZI SITA HADI MIAKA MITATU.

heroby said...

hahahahaha
jamani poleni sana ,ila kiukweli wasichana wakazi wanasumbua sana ,mbaya zaidi wakitaka kuondoka huwa awasemi mapema unashangaa hasubui unajianda kwenda kazini mtu anakugongea mlango eti anakuaga ,ivi uwa wanaakili kweli .basi hapo ndo unapo changanyikiwa ,ndio maana siku izi kuna day care jamani utakuta katoto kadogo kana miaka miwili kamebeba begi kanapakiwa kwenye school bus kanaenda kupoteza mda uko yote hii coz ya wafanyakazi .

Anonymous said...

Nadhani baada ya kukipata hicho ulichokiita cha moto kwa weekend moja, ujue ndio mfanyakazi wako wa ndani anakipata kila siku hapo kwako. Hivyo ni vema kuangalia utaratibu wa maslahi na jinsi unavyomjali. Wafanyakazi wa ndani na wao mara nyingi huwa wanareact kutokana na jinsi unavyomchukulia, kama wewe ni mtu wa mdomo sana watakukimbia sana, wanaweza kuja leo wakaaga kesho. Binafsi sina matatizo na wafanyakazi wa ndani hata siku moja na hakuna hata mmoja anayeishi chini ya miaka miwili kwangu. Huwa akija namuangalia jinsi anavyolea mtoto na wakati huo huo naangalia ni jinsi gani nitamsaidia ili akitoka kwangu asiende kulea mtoto sehemu nyingine, aende kwao kujitegemea hivyo nae pia namtafutia maisha yake. Wote huwa nawatafutia sehemu wanajifunza kushona nguo, akimaliza namnunulia cherahani, then atakapotaka kuondoka tunaagana kwa amani kabisa tena anasubiri mpaka nimeleta mwingine anamfundisha kazi ndio anaondoka na cherahani yake kwenda kuanza maisha. Nafanya hivyo kwa vile nafahamu wamekuja kufanya hiyo kazi sio kwa vile wanapenda sana, bali ni kwa sababu wanahitaji kujikimu, sasa ni bora kuwasaidia ili wakaweze kuendesha maisha yao ya baadae na kama wakienda kucheza iwe ni kwa kosa lao. Hawa ni binadamu wenzetu, unapokuwa nae kitu muhimu sana usimkope mshahara wake, pamoja na kwamba anakula kwako, mwisho wa mwezi ukifika mpe pesa yake kamili atajisikia unamjali sio biashara ya kukaa na pesa yake kwa hoja kwamba unamtunzia hilo linawaumiza kichwa. Pia ninyi mnaobadilisha kila wadada kila kukicha mnawaharibu watoto wenu, inawezekana vipi kwa mwaka mmoja wadada sita na bado unadhani matatizo ni yao tu? lazima nawe una tatizo lako ndio maana wanakukimbia, na tatizo kubwa sana kwa wanawake wengi ni dharau, hao wadada ukimdharau kwa lolote atakukimbia tu. Ni huo tu mchango wangu.

Anonymous said...

Hongera kama hao madada hawakutesi na unaishi nao hivyo.
Hivi nakuuliza kuna mtu anayeweza kumtesa mtu anayebaki na mwanaye zaidi ya masaa 2?
Unaondoka kwako saa 12alfajiri unarudi jioni saa kumi. Vipi umtese dada wa mwanao?
-Je naye akitesa mwanao ukiwa hupo?
HAO MADADA NI WAKOROFI TUUUUUUUUUU

Anonymous said...

yep, hawanitesi mimi wala watoto na naishi nao vizuri sana. ndio kuna watu hilo hawalijali kabisa. Mtu unalelewa mtoto na bado mdada anakuwa kama yupo jela vile, nasema hivi kwa vile nimeshuhudia kwa macho yangu.

Anonymous said...

Poleni sana wenzangu kwa shida ya dada wa kulea watoto. Ninashauri sasa hivi ni muhimu kuwepo day care. Shule za Kata zinasaidia sana wasichana kuweza kusoma hadi F4. Nadhani mtu akiweza kufungua daycare center nzuri watu watapeleka watoto tuu. Ila shida kubwa nadhani ni kazi za ndani, kufua, kudeki, kupika etc. Hapo nadhani inabidi wazazi wote wasidiane kutunza familia.. Penye nia pana njia, tutafika tuu.

Jiang, fungua day care watu tulete watoto hapo!!

Anonymous said...

kwa wale ambao wanaishi nchi za nje na familia hamna wasaidizi wa nyumbani kila kitu mnafanya kusaidiana wewe na mume wako kama ndio mtoto kazaliwa na huko nje kumbukeni mara nyingi hamna ndugu kama wa bibi wa aunti wadada nk ni wewe na wewe tu. kama ulikuwa unafanya kazi unachukua off mtoto akizaliwa wakati huo mnapanga mkakati kama utaacha kazi kwa muda kuwa mama wa nyumbani mpaka hapo mtoto atakopofikia umri wa kwenda day care ila kufua kupika nyumba usafi kulea ni nyie wenyewe hamna house girl wala nini ni ngumu lakini mkizoea less headaches ndani ya nyumba lakini hii inahitaji ushirikiano sana wa mume huwezi kufanya hii kama mume anakuachia kila kitu wewe peke yako

Anonymous said...

jamani hili janga ni kubwa sana,mimi nilikuwa nao wawili mmoja wa mtoto na mwingine wa kazi za ndani yani nawadekeza nakuwanyenyekea lakini wapi kazi yao ni TV yani natamani mwanangu akue tu nimpeleke daycare manake naona nitapata ugonjwa wa moyo manake kuwagombeza naogopa wasije kunifinyia malaika wangu.

Jiang said...

Mdau mwenye bahati ya kukaa na wasichana miaka miwili hongera sana, kwa kweli hiyo ni bahati!
maana kama unavyoona comments za wadau wengine, sidhani kama sisi wote tutakua tunawatreat hawa wadada vibaya, wakati tukijua kwamba ndio wanaoshinda na watoto, ingawa sikatai kuwa kuna wanaowatreat hawa wadada vibaya.
Kiukweli mi nimejitahidi kuwafanya kama wadogo zangu, ila wanaishia kuondoka tena kwa vituko, kuna mmoja alikua mzuri sana, maana alikua ana uzoefu, siku moja wakati naondoka mtoto ananililia, nilisahau kitu nikarudi ndani, nikakuta anamgombeza, 'nyooo, unamlilia kwani ndio unashinda nae huyo'sasa pata picha nilijisikiaje kusikia mwanangu anaambiwa hivyo kwa kufanya kitu cha kibinadamu kabisa, kumlilia mama yake wakati anaondoka.
tunavumilia mengi sana kwa hawa wasichana, maana hata kuwagombeza tunaogopa, ila kwa kuwa wanaofanyiwa ni wanetu, uvumilivu unakua mgumu, kwa sababu kwa mtoto ambaye haongei, hata hawezi kukuambia anayofanyiwa wakati haupo, ila ukirudi ghafla siku moja unaweza ukakuta kituko kikakutoa machozi!
pia hawa wasichana hawachukulii hii kama kazi, ambayo inaweza kumtoa hatua moja kwenda nyingine, hawaangalii mbele, na hawaoni kuwa ndio inayowaweka mjini, la sivyo wangekua wanaijali kazi yao.
kwa kweli naona solution ya kufanya wenyewe kila kitu ni muhimu, kama wikend niliyoshinda na X peke yangu, babamtu alikua anakarangiza, sisi tumeshazoea hivyo!tatizo ni hizi kazi zetu wengine, kurudi home saa 3 usiku, kusafiri mara kwa mara...
Kuhusu kuanzisha Day care, hata sifikirii kabisaaaaaaaa!

Anonymous said...

uyo mama anaekaa na wadada miaka 2 yeye ajisemee mwenyewe ok ata km kuna hao wachache alioona ni hao,,,watu tunasota na hawa wadada adi unajiuliza ivi nimfanyie nn anielewe?maana huchongi mdomo,unampa pesa yake NZIMA,analala pazuri tu,wamtibu,anakula na nyie meza moja chakula ichoicho,kazi ukiwepo unafanya pia na wewe humuachii afanye vyote yani kwa ufupi humbagui,,,ila kituko atachokufanyia unachoka na roho yako...ni wa kuwaombea sana wengi wanakua na mapepo kabisa ya izo tabia za kifedhuli,,,yani tuwe serious kuombea wadada hawa.
me my sista aliacha kazi mwaka na nusu kabisaa akae home alee watoto ebu fikiria jaman na elimu yako na kazi zuri weeee,mabibi nao cku izi wanabiashara zao huwezi mwachia mjukuu