Monday, February 8

Hasira za watoto

Huyu mdau niliambia anadeka, kalia, kajigalagaza chini weeee, hamna aliyehangaika nae, ma'mtu wala hakua anamwangalia, mwisho akaamua ajinyanyue mwenyewe, akanyamaza na kuendelea na shughuli nyingine!


Hii ni tabia ya kawaida kabisa kwa watoto, hasa wa miaka miwili, kwa kiingereza inaitwa 'tantrum' kulia ghafla bila sababu ya msingi, na kujigalagaza chini ndio zao, hasa sehemu za watu wengi.
Inatia hasira sana kwa mzazi, ila na wewe ukikasirika na kuanza kumgombeza haisaidii kitu, maana wote mtakua mnapiga kelele, afu mzazi ndio utaonekana mjinga, unachotakiwa kufanya ni kuwa mtulivu na kujaribu kumtuliza mtoto kwa sauti ya kawaida bila kutumia hasira, kama kuna kasababu na unaweza kukatatua, basi katatue ili mtoto atulie.

2 comments:

Anonymous said...

Hapa Jiang umesema! Tena hata wakianguka unatakiwa umuangilie kama humuoni vile(ili kuwa na uhakika hajaumia)!! akiona hamna aliyemsemesha anaamka na kujifanya kama hajaanguka vile. lakini ukianza pole, basi kilio hapo!!!!!

disminder

Anonymous said...

Umenikumbusha Mwanangu mimi ndo zake kwakweli huwa nakaa kimya! analia anajigalagaza chini, anajikojolea then ana chapa usingizi, akifikia hapo namdaka naenda kumlaza.

Alishaacha kujikojolea tangu akiwa na miezi 10 lakini hasira za kudeka ndo ananitisha.