Sunday, February 7

X hair cut

Mi nilikuaga naona tu watu wanabebana wanaenda salon kunyoa, wakirudi wamependeza naishia kuhadithiwa yaliyojiri huko.
Kabla sijaenda Dodoma nikaamua nikashuhudie yanayotokea, maana nilikua siamini kama mdau anaweza kutulia, kukata kucha tu kwa kutegeana...
Kumbe siri ya mafanikia ni hicho kiti cha gari, mdau yeyote akishawekwa hapo, ananyolewa bila tatizo...hii ni BM Barber Shop, Kinondoni.

Baba alikua kule kwa mbali naye akipendezasha kichwa...hicho kigari kinatoa milio, so mdau anazubaa hapo akiendesha gari...

...ila pia mnyoaji anatakiwa awe makini, maana dereva anaweza akakata kulia, wakati mashine iko kwingine...

Alivyomaliza badala ya kuogeshwa kichwa kama wakubwa yeye alifutwa tu na taulo...

Hapo vipi...?
Ila nimeambiwa kuna wadau wakishamaliza kunyoa hawataki kushuka kwenye kiti...hapo sasa!

3 comments:

Anonymous said...

Aaah kwa hicho kiti? hata kama ni mimi nataka nikatwe nywele siku nzima.


disminder

Anonymous said...

mmh thats good idea
kama unaweka vitu kama hivyo basi ametupata na pia asante mama X kwani hicho kijiwe nakisifu kwa kuboresha huduma wa watoto maana justice wangu alikuwa akienda pale tangu anaaanza hadi anamaliza ni kulia tu mtindo mmoja hadi nikanunua machine yangu!1 nitampeleka siku moja akajinafasi!! ila swali langu ningependa pia watenganishe mashine kwa ajili ya watoto na watu wazima kiafaya sasa hivi inakuwa ngumu jamani!!

nawapenda wazazi na watoto wote

friend & mom of 2jjs

shamim a.k.a Zeze said...

Nimewapenda ni wabunifu mnoooo