Saturday, February 6

Hati punguzo!

Huku mjini naona haijashika kasi, nilishangaa nilipofika nje kidogo ya Dodoma mjini na kukuta foleni ndefuuu, na hii ilikua jioni, kuna waliohudumiwa asubuhi...hawa wote walikua wanasubiri vyandarua vyao vya Hati Punguzo.Foleni ndio ilikua kama hivi...usipoenda na mtoto hupewi chandarua!

Mdau akipiga mahesabu ya kubeba chombo chake...

Kitu mkononi...mbu bye, bye!
...chandarua cha Olyset, chenye dawa ya kudumu muda mrefu ya kufukuza mbu!
Tunaweza kulaumu kwa mengi tu, ila penye kusifia acha tu tutoe sifa, katika hili serikali imefanya kitu cha maana.

1 comment:

Dorah said...

Hello Jiang, asante kwa kutuonyesha zoezi la chandarua. Je unaweza kunitajia ni dawa gani iliyowekwa kwa ajili ya kuzuia mbu?
Nitashukuru kwa msaada wako.