Monday, March 1

Jihadhari na madada wachawi....


Hii nimetumiwa na mdau Fatuma Mmbaji:
Jamani kama mlivomsikia mchungaji jana kwenye ibada ya asubuhi Azania Front…. Kila ukimpokea msichana wa kazi unatakiwa kufanya “SPIRITUAL CHECK UP” – yaani ufanye maombi kwanza na kama amekuja na nguvu zake za giza zishindwe kwa jina la YESU.

Someni hapa chini….


Mfanyakazi ya ndani anayedaiwa kuwanga akiwa katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungu (UBT) tayari kusafirishwa kurejeshwa kwao Morogoro baada ya tuhuma hizo za kuwanga, abambwa na ndumba kibao na ungo
  • Asimulia mambo ya kutisha
  • Maombi yasaidia kumnasa
VITUKO simanzi vimetawala nyumbani kwa Mzee Naftal Chacha (60), mkazi wa Ukonga ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), baada ya hausigeli wake, Odillia Mikka (15), kukutwa chumbani kwake akiwanga huku akiwa amekaa ndani ya ungo.

Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza katika nyumba hiyo baada ya mtoto wa mwenye nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Miriam Naftal kumkuta msichana huyo akiwa amechuchumaa ndani ya ungo uliosheheni ndumba kibao pamoja na nguo za ndani za mtoto mkubwa wa kike wa familia hiyo.

Miriam baada ya kuingia katika chumba hicho ghafla alianza kupiga mayowe kumshtua msichana huyo ambapo familia nzima iliyokuwamo ndani ya nyumba hiyo iliingia chumbani huko ili kujionea kinachoendelea.

Baada ya kufika umati wa watu walimshuhudia hausigeli huyo akiwa ameshikwa na butwaa na walipomhoji alidai kuwa amechukua nguo za ndani za msichana wa mwenye nyumba huyo, Bhoke Naftal, ili azipeleke kwa bibi yake anataka kumuua kwa kumuweka msukule.

Kutokana na kauli hiyo mwenye nyumba hiyo ambao ni Wasabato walianza maombi ndipo hausigeli huyo aliyefikia nyumba hiyo Desemba 24, 2009, alipoanza kujieleza mambo mbalimbali anayoifanyia familia hiyo kwa kushirikiana na bibi yake anayeishi kijiji cha Kitete mtaa wa Yangeyange Morogoro.

Hausigeli huyo alidai kuwa tangu afike katika nyumba hiyo bibi yake amekuwa akija usiku na hutembelea vyumba vyote vya nyumba hiyo na kuichezea familia nzima.

Amesema kazi hiyo aliinza tangu akiwa na umri wa miaka minne ambapo mafunzo hayo aliyapata kwa bibi yake ambapo tangu aanze amefanikiwa kumuua mtoto mdogo wa miaka miwili wa tajiri yake mmoja anayeishi Morogoro ambaye hadi sasa wamemuweka msukule.

Ameongeza kuwa alimuua mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miezi mitatu ndani ya nyumba hiyo. Baada ya kukiri kufanya kitendo hicho, wanafamilia ya mtoto huyo walimpiga na kumtimua kazi bila ya kumpa hata senti tano.

*****

Habari hii nadhani ishatoka kwenye magazeti pendwa, ila aliyenitumia hajaniambia ni lipi, kwa ufupi ndio hivyo, inadaiwa huyo dada  amefanya vituko vingi vya kichawi...
Tujihadhari na kuchukua wadada tusio wajua, maana hata kama si mchawi anaweza akawa anamfanyia mtoto vitu vya ajabu, cha muhimu zaidi ni kumtanguliaza Mungu wako mbele, kama mdau alivyosema, spiritual check up, maana mengine huwezi kuyaona kwa macho yako ya kibinadamu!

4 comments:

shamim a.k.a Zeze said...

Mh inatishaaa

Anonymous said...

mambo haya!! jamani nyumba hizi zina mengi.
ee Mung wanusuru watoto wetu!

disminder.

Anonymous said...

VERY TRUE, KILA UNAPOTOKA HOME NA KABLA HUJALALA HAKIKISHA UMEKABIDHI WANAO KWA MENYEZI MUNGU.

SIO HOUSEGEL TU HATA HUKU MASHULENI BARABARANI, TUKABIDHI KWA MUNGU KILA SIKU JAMANI

Mama Kelvin said...

Jamani hili naliamini na tunatakiwa pia kuwasachi mahouse girl wetu wakifika tu, pia kuwashtukiza kurudi nyumbani, mimi kuna rafiki yangu mmoja alinisimulia msichana wake wa kazi huwa anajibadilisha chatu watoto wanamchezea wanacheka sana mpaka majirani wanashangaa ilibidi mama afanye uchunguzi akarudi mida ya mchana akaa nje muda ukafika watoto wakacheka sana basi dada akachungulia dirishani akaona chatu hakuamini anacheza na watoto basi alivyofungua mlango wa nche akageuka dada tena basi ikabidi awambie majirani akashauliwa amulize akaeleza kila kitu dada basi akampandisha gari kuondoka, yaani nimesikia mambo mengi juu ya wadada. ushauri tujitahidi kujua chimbuko la dada tusiokote tu sababu ya shida pia tumkague akija, pia kumlazimisha kwenda nae kwenye maombi mara moja moja nae ukiwa na nafasi .ili kama kunachochote utajua huko.Asante mdau kwa maada hiyo