Wednesday, May 5

Aurelia's birthday party

Jumapili iliyopita ilikua birthday party ya mdau Aurelia Croft ambaye alitimiza miaka mitatu Alhamisi.
Party ilikua home kwao Mbezi, kama nilivyoahidi, ingawa kwa kuchelewa kutokana na uzembe wangu(naombeni mnisamehe kwa hili), picha hizi hapa!


 Birthday girl Aurelia alitoka na kivazi cha toka India, kuna jina anakiita nimesahau...

 
 Full kiko hivyo! Hiyo top imeshonewa shanga zinang'aa ile mbaya, hasa usiku! Mi nilikipenda sana hicho kivazi, afu mwenyewe alikua anaringa nacho...

 
Ma'mtu, Upendo Hartsuiker akileta tam tam...
 
 Mdau alifurahia hiyo tam tam mno, afu alivyokua anaimbiwa happy birthday, ndio kabisa, akaona dunia yote yake, alifurahi sana!...akipuliza mishumaa mitatu...

 
kata keki tuleeee...
 
 ...akimlisha daddy...

 
 ...bibi...

 
 Xchyler alikuwepo sana eneo la tukio, ila ubize wooote aliuhamishia kwenye maji, afu siku yenyewe ilikua na mvua, so no kuogelea, lakini aliloa,  na kidogo adumbukie kwenye maji!

...Hii birthday party walialikwa watu wachache sana, wadauwalioalikwa wanne tu....huyu anaitwa Cenzo (sijui ndio inavyoandkwa???)

...Junior na mama...Junior ana miezi mitatu, m-cuuuuuute, hamna mfano!

...mdau mwingine aliyekuwepo ni Harrieth, hapa nawasukuma kwenye baisikeli...moja ya zawadi toka kwa wazazi wa birthday girl...

...Hapa wadau wamekusanyika wanapaka rangi, zawadi hizo zilishafunguliwa, am sure kuna rangi zilipotea kabla party haijaisha!

Ilikua kazi sana kupata picha ya X, maana alikua hatulii sehemu dakika moja ikaisha! 
Hapa yuko na Daddy anajifunza kuchoma mishkaki...party ilikua barbecue style, Six alikua ndio mkuu wa idara ya mishkaki!
Party ilifana sana, ndogo lakini ilikua bomba!

1 comment:

Bazizane said...

Mashallah baba X anavutia sana, hongera mama X kupata mume wa shoka.