Friday, July 30

Mfanyakazi wa ndani anyonga mtoto

Mfanyakazi wa ndani (dada/yaya) amenyonga mtoto wa miaka miwili (2) aliyekua akimlea, Seth Steven, huko maeneo ya  Uwanja cha Ndege, Morogoro amenyongwa na baadae naye alijinyonga baada ya kufanya
kitendo hicho. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Thobias Andengenye, aliwaambia waandishi
wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumatano saa 2.45 usiku katika nyumba ya Steven Kapombe alipokuwa akifanya kazi za ndani. Andengenye alimtaja mfanyakazi huyo kuwa Zaina (16). 

Alisema Zaina anadaiwa alianza kumnyonga mtoto huyo kwa kutumia kipande cha khanga na baadaye kujinyonga mwenyewe kwa kutumia kipande hicho hicho cha khanga. Kamanda huyo alisema chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika, na kwamba  polisi inaendelea na uchunguzi. 

Habari zisizo rasmi zinasema kuwa mdada huyo alishaambiwa kuwa afungashe virago vyake, tayari kwa kuondoka na waajiri wake, ambao ni wazazi wa mtoto huyo.

Mama na Mwana inatoa pole kwa mama, baba, ndugu na jamaa wa mtoto huyo, kwa kupatwa na msiba huo.
Kwa tukio hili, Mama na Mwana inawasihi wazazi wazidi kuwa waangalifu juu ya watu wanaowalea na kuwatunza watoto wao, kwa kujua wanakotoka, historia na tabia zao kwa ujumla. Pia kwa usalama zaidi pale unapomtaarifu kwamba anaondoka, usimpe majukumu mengine tena hadi atakapoondoka, maana anaweza hata akaweka sumu kwenye chakula, kutegemea na akili yake. Pamoja na hayo, Mama na Mwana inawakumbusha kuishi vizuri, kwa upendo na ustaarabu wadada hawa kwani ni watu muhimu sana kwenye maisha yetu, na hasa ya hao malaika wetu.

1 comment:

Anonymous said...

ni kweli mama x, watu tujifunze vizuri kuishi na wadada wa ndani. watu wengi wamekuwa wakiwanyanyasa hawa viumbe wakati ni watu muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Ebu fikiria wewe siku nzima uko ofisini nyumbani umemwacha huyo dada na mtoto na ndie anayepika chakula chenu, akiamua kuweka sumu. Wakina mama wenzangu tujifunze kuwapenda wadada. mimi namshukuru mungu toka niko kwa wazazi mama alikuwa anawalea wakina dada utafikiri ndugu wa damu, na mimi nimefata kama mama, nampenda sana msichana wangu wa kazi.