Tuesday, October 5

Malselino akisaidia kufua kwa aina yake


Mdau amenifurahisha sana...anaitwa Malselino...
 Aliyaona yametulia kwenye beseni...sijui ndio wanasubiri kusuuzia nguo...anyway, mipango yao na hayo maji haimhusu, maana naye ana mpango wake...


...anapima temperature, yasije yakawa ya moto bure.......hapa ashayapatia, anayachezea sana tu...

...mikono tu...na mguu ndani!

 mmmh, taratiiiibu!


...kiutaalam mdau kaingia bila kuanguka na beseni!
...mdau kama Malselino mimi huwa namwita janjaful!.

Mission accomplished.

...kama yalikua ya kufulia halafu maeneo ya tabu ya maji kama Kimara hii inakua imekula kwa mfuaji...
(Thanks Anko A Ruta kwa picha)

4 comments:

Anonymous said...

ANGALIZO KWA MAMA WA MTOTO HUYU: ASIONE SIFA MTOTO KUCHEZEA HAYO MAJI HIVYO NINA MFANO HAI WA MTOTO ALIWAI KUFA KWA MCHEZO HUU KAMA HAMNA MTU KARIBU MTOTO HUYO AKIINGIA VIBAYA AKALALA CHALI ATAMEZA HAYO MAJI NA KUFA HIVYO SI SIZURI KUMUACHA AFANYE HAYO. THANKS

Anonymous said...

SIO JAMBO LA KUFURAHISHA HATA KIDOGO, NI HATARI SANA SANA, UKIJISAHAU DAKIKA 2 TU AKILALA CHINI YA HAYO MAJI NI HADITHI NYINGINE ITAFUATIA,

mama wawili said...

mchezo huo hatari sana hasa kwa watoto chini ya miaka mitatu so akina mama tujitahidi kuweka maji ya ndoo au dishi mbali na watoto

Anonymous said...

Hii ni hatari kubwa tena sana, watoto wa umri kama huu na hata 5 yrs wanakufa kwenye ndoo za lita 20 tumewashuhudia baadhi. Please Mama na Mwana weka darasa kuhusiana na tabia hii, liwafundishe na wengine wasiojua madhara yake. Mzazi huyu ataona sawa kwa kuwa alikuwa karibu na anapiga picha akumbuke mtoto atafanya hivi siku nyingine punde aonapo maji na on absence ya watu wazima. Please Mama na Mwana tumia picha hizi kuwaelimisha na wazazi wengine waache kabisa kurisk namana hii na maisha ya watoto.
Mama Hope