Thursday, November 25

Mtoto azaliwa ubongo nje Morogoro


Kichwa cha mtoto huyo kinavyoonekana

Mtoto mmoja amezaliwa ubongo ukiwa nje baada ya kukosa ngozi ya kichwa huku akiwa mwenye afya njema katika hospitali ya Wilayani Ulanga mkoani Morogoro .
Mtoto huyo wa kiume aliyezaliwa siku ya jumatatu majira ya saa tatu usiku,
atampelekwa katika hospitali kubwa mkoani Morogoro kwa uchunguzi zaidi wa nini kifanyike kukabiliana na tatizo la mtoto huyo ambaye hadi sasa yupo hai na afya njema.

Matroni wa wodi ya kina mama bi. Haule akimhudumia mtoto na aliyembeba ni Bi Sabina Lyombo mama wa mtoto

Kaimu Mganga Mkuu (W) Dkt Amani Kombe amesema  kuwa hali ya mtoto kuzaliwa na kukosa ngozi ya kichwa hutokea wakati wa uumbaji wa viungo mbalimbali vya mwili wa mtoto na hali hiyo huweza kusababishwa na ukosefu wa madini mbalimbali kwa mama wakati wa ujauzito aidha ni tukio la kwanza kutokea katika hospitali hiyo ya wilaya.
Mama wa mtoto bi. Silvia Lyombo (20) ambaye ni ujauzito wake wa kwanza alisema kuwa hakupata matatizo yoyote ya kiafya wakati wa ujauzito na alijifungua katika hali ya kawaida mtoto mwenye uzito wa kilo 2.9 na kuwa ananyonya kama kawaida na hana tatizo lolote zaidi ya kukosekana kwa ngozi ya kichwa aidha hakuna dawa zozote ambazo alizitumia katika kipindi chote cha ujauzito wake.

1 comment:

Anonymous said...

mwacheni mungu aitwe mungu. Namwombea.