Friday, May 25

Binti zetu...

Usiogope kusikia binti, wakati ndo kwanza mwanao ana miezi saba kama Cleopatra wangu, Yessss miaka kadhaa ijayo watakuwa mabinti warembo wenye kujitambua na kujipenda.

hawa wako kama wadoli...unapenda binti yako awe kama mdoli-doli? au ...
Je umemuandaaje mwanao wa kike ili atakapokuwa binti awe jasiri na mwenye kujiamini?
Je umeshawahi kuwaza unajipangaje kumjengea mwanao wa kike ujasiri na kujiamini?
bofya hapo kushoto tujadili hili...

Asikwambie mtu hivi ni vitu muhimu sana ambavyo mtoto anatakiwa kujengewa ili hata akiwa mtu mzima isimpe shida.

Sio wa kike tu bali hata wa kiume ingawa wao tutaweka mada yao itakayojitegemea.
Ni muhimu watoto wetu wa kike wajitambue. Hii itamsaidia baadaye kukabiliana na changamoto za makuzi ambazo zitamkabili. Mtoto wa kike ajengewe kujiamini, kujithamini na kujipenda. Ajue ni vitu gani kama msichana anapaswa kuwa navyo katika chumba chake cha kulala na kwenye dressing table yake kama anayo.

Mafuta, mswaki, dawa ya meno na vingine. Pia unaweza kumuandalia kipochi chake kidogo ambacho kinaweza kuwa na vitu kama hivyo ili hata anapoenda kwa ndugu, jamaa na marafiki awe na vitu vyake vya kutumia.

Hapa ndo utakuta mtoto anapokuwa binti anapenda kujiremba, mwache mtoto ajirembe jamani as long as ana tabia njema na anajiamini haitampa shida. Ila pia urembo usizidi umri, sio mtoto wa miaka mitatu ashakolezwa wanja hadi sikioni, lipstick nyekunduuuu - dah, ikipitiliza nayo si nzuri!
Ila hata akiamua kuwa si mtu wa kujiremba, yaani tomboy flani poa pia, as long as anajiamini na anajua anachotaka kwenye maisha yake na ma'mtu kama role model wake unamwongoza vizuri kufikia dreams zake!

NB: Usimkataze mtoto kufanya kila anachokipenda kama hakina madhara. Nakumbuka mimi wakati nipo mdogo kwenye jamii iliyotuzunguka kulikuwa na imani kuwa mtoto anayejipodoa atakuwa ana tabia mbaya na atakuwa anaringa. Hii imeniharibu hadi leo kuwa mtu asiyejiremba, ingawa nawatamania watu wanaojiremba, ila kwa ajili si tabia niliyokua nayo inanipa shida kuifanya. Nipake poda sawa, nisipake sawa. Wanja nikipaka twende nisipopaka hakuna kitachoharibika...ila wanaopaka kila siku nawazimia mno. I wish ningekua na moyo wa kupaka kila siku.

1 comment:

Anonymous said...

Thanks kwa kutuelimisha coz nimepata kitu ktk kulea kwa kwakweli! Ubarikiwe.



Mama E.