Saturday, May 5

CCBRT inafanya miujiza kwa wanawake wenye fistula

Imagine kuvuja mkojo saa zote bila kuwa na uwezo wa kuzuia... zaidi ya hapo, unavuja mkojo na kinyesi bila kuwa na control? Utajisikiaje? Mwisho wa dunia!!!
wagonjwa waliopona na wanaoendelea na matibabu ya fistula wakiimba...




Hiyo inaotwa fistula, ambayo inatokana na complications za uzazi. Na nikikuambia it can get worse? kupata matatizo yote hayo, na mtoto akazaliwa amekufa!!! Juu ya hapo kutengwa na jamii, kuachwa na mume, na kuishi na tatizo hili kwa miaka 20!!! Kwa kweli chozi lilinilengalenga!
Tatizo la fistula linawakumba kati ya wanawake 2,000 hado 3,000 nchini kila mwaka. Wanaotibiwa hawafiki 1,000!- Yes, watu wanakaa na fistula hata hadi miaka 40, ingawa inatibika!

...hawa wenye khanga hapa mbele ndio waliopona.....huyu ni mfanyakazi wa CCBRT akiwaelekeza jinsi ya kuishi baada ya matibabu...

Ijumaa (jana) nilitembelea hospitali ya CCBRT (kikazi) na kuwaona akinamama, wengi wao wasichana wadogo. Hapo CCBRT wanatibiwa bure. Nilifurahi kuona wanapata huduma hii, ila challenge ni kuhakikisha kinamama wengi zaidi wanafikiwa na huduma hii.

Niitawahabarisha fistula ni nini, na ntawaeleza jinsi wanawake wenye tatizo hili wanavyoweza kufikia matibabu - inaweza isikutokee wewe, ila unaweza ukawa unamfahamu mtu mwenye tatizo hilo ukamsaidia kwa information - matibabu ni BURE!

...kama unataka taarifa zaiadi ingia kwenye website ya CCBRT

1 comment:

Anonymous said...

Inatia huruma sana kuona akina mama wanahangaika na huu ugonjwa. Nadhani kitu kikubwa ni uelewa katika jamii yetu ni mdogo, kungekuwepo na uhamasishaji kuanzia vijijini kuhusiana na huu ugonjwa ili mtu akiona dalili kama hizo anawahi hospitalini.

Elimu ingetolewa kwa wote hasa wanaume pia kwani wao nao ni tatizo pindi mwanamke atakapomuelekeza tatizo hili ndo vita itakapoanza kuwa kaupata wapi au kuanza tiba za kienyeji baada ya kuwahi hospitalini.

Mara nyingine tena akina mama wakipatwa na magonjwa wanajificha kwanza kutokana na kuwa na elimu ndogo ya mwili wake, kutokuwa muwazi kueleza tatizo.