Siku hizi karibia nyumba nyingi sana zina house girls na hawa huwa muhimu sana katika kutuangalizia nyumba zetu na watoto wetu haswa pale tunapokuwa hatupo nyumbani, na siku hizi nyumba nyingi huwa na house girl wawili yani mmoja kwa ajili ya watoto na mwengine kwa ajili ya nyumba kwa ujumla, sasa basi huyu house girl wako ulimpataje? unapajuwa kwao? ama ndio wale tu tunaoletewa kwa kupigiwa simu na sisi kwavile tunawahitaji sana tunawakaribisha nyumbani kwetu bila hata kutaka kuwajuwa kwa undani sikia mkasa huu..
Kuna familia moja ndio kwanza walikuwa wameoana na wanamtoto mmoja hii familia ilihitaji msichana wa kazi kwasababu wote walikuwa ni wafanyakazi ili aweze kukaa na mtoto, basi tafuta huku na kule siku moja yule mama akaambiwa kunamsichana wa kazi kijijini singida tuma hela apakiwe kwenye gari aje, basi kwavile yule mama naye alikuwa na shida wa msichana kweli kwa haraka bila kuchelewa akatuma hela yule msichana akapakiwa kwenye basi baada ya siku tatu akawasili dar.
Yule mama akampokea na kukaa naye vizuri kama ndugu yake yani hakuna ambalo jema hakumfanyia yule msichana maana yule dada kweli alikuwa anajituma sana katika kazi zake yani watu walioingia ile nyumba walimtamani sana yule dada, miezi sita ikapita yule dada wala hakubadilika katika utendaji wake wa kazi.
Basi siku moja hivi yule mtoto wa mama mwenye nyumba akaumwa ghafla wakamkimbiza hospital, walipomfanyia uchunguzi wakabaini alikuwa ana food poison ndio maana alikuwa anaumwa sana mpaka kuishiwa nguvu maana anatapika sana pia, basi akapata matibabu na kupona lakini cha kushangaza yule mtoto alikuwa akipata hayo matatizo kila mwezi mara kwa mara, wazazi wake wakiwa hawaelewi ni kwa nini.
Kumbe bwana matatizo yote anayasababisha dada wa kazi yule dada alikuwa anamtindo kila mwezi akiwa katika hedhi hukamulia damu zake za hedhi kwenye chakula cha mtoto (hayo ni maagizo aliyopewa kutoka nyumbani kwao singida) na hayo aligundua jirani ambaye alisikia mtoto akilia bila kunyamazishwa kumbe dada alikuwa busy na kazi yake kwahiyo yule mama kuchungulia dirishani ndio kumuona dada akifanya hayo, japo walimueleza mama wa mtoto yeye hakuamini aliona ni wivu tu na maneno wanayompa kuhusu msichana wake ili aondoke maana wanajuwa jinsi alivyomchapa kazi.
Basi ugonjwa wa mtoto kila mwezi ukawa unaendelea wameshamaliza hospital za kila aina, lakini wakati wote huu yule mama bado alikuwa anawaza maneno ya yule jirani yake aliyomwambia, siku akamuuliza dada kwani lini huwa unapata hedhi maana nataka nikununulie pedi, dada si anajuwa hamna anayejuwa siri yake akamueleza yule mama kweli kesho yake akamletea pedi sasa akawa anasubiri na yeye ajionee kama ni kweli.
Basi akaomba likizo ofisini kwake ya wiki na kupewa lakini nyumbani akawa anaondoka asubuhi kama anaenda kazini lakini alikuwa akiishia kwa yule jirani ikafika saa sita muda ambao mtoto hula chakula cha jioni, kama kawaida yule mtoto akaanza kulia wakachukuana kwenda mpaka kwenye dirisha la sitting room na kuchungulia yule mama alivyoona msichana wa kazi anachokifanya akazimia hapohapo ndio dada kushtuka na kwenda nje baada ya kusikia kishindo.
Mara kumuona boss wake akaanza kupiga kelele kwamba anataka watu wamsaidie ndio watu kuja pamoja na jirani kumchukuwa kumpeleka hospital, yule mama akamwambia dada abaki amlishe mtoto wakati huo dada bado hajui kama alishaonekanika yule mama akatibiwa na kurudi jioni na mumewe njiani akawa ameshamuhadithia mumewe ile story nzima na akamwambia kama alishaambiwa na yule mama jirani sema hakuamini, yule baba alijawa na hasira sana na kutaka kwenda kumpiga yule msichana lakini wakashauriana kwasababu yle hajui kama tunajuwa basi tusimuendee kwa vurugu tumuite na yule mama shahidi tukae na yule dada tumuhoji.
Walipofika nyumbani kwa kujikaza wasipandwe na hasira wakamuita dada pamoja na yule mama jirani wakamueleza dada yote wanayoyajuwa, basi yule dada ndio akaanza hekaheka za kuogopa, na kuomba masamaha walipomuuliza kwanini alifanya hivyo na kwa muda gani ndipo akawaambia kwamba tokea siku ya kwanza mtoto alipoanza kuumwa, na kwanini alifanya hivyo akawaambia ndio alivyofundishwa na mama yake mdogo huko kijijini aliyemlea ambapo huyo mama naye alikuwa msichana wa kazi kwenye nyumba ya watu akawa anafanya kazi vizuri na kupendwa sana na wenye nyumba na baadaye mpaka kutamaniwa kimapenzi na baba mwenye nyumba ndipo alipoamua kufanya hivyo akawa anakamulia damu yake ya hedhi kwa mtoto mara kwa mara yule mtoto akaumwa mpaka kipindi akafa, na mtoto wa pili pia ikafika wakati akawa anapika chakula tofauti kwakuwa baba mwenye nyumba alikuwa anachelewa kurudi nyumbani kwahiyo chakula chake huwekewa kwenye hotpot zake mpaka akija ndio hutengewa basi chakula anachokula mama naye akamfanyia hivyohivyo na baadaye kumuwekea sumu na kufa na kwakuwa chakula cha wenye nyumba na watu wengine wa kazi kwenye ile nyumba huwa hakipikwi pamoja basi ilikuwa rahisi sana kwa yeye kufanya vile kwahiyo akabaki yule baba kwakuwa walishaanza uhusiano wa kimapenzi akageuka sasa kuwa mama mwenye nyumba huko singida na mpaka leo kwahiyo alivyopata yeye kazi dar es salaam alishauriwa kufanya hivyo na yeye apate nyumba yake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mmmeona balaa za hawa wadada jamani, basi yule dada akapelekwa polisi akafunguliwa mashtaka na baadaye mahakamani akafungwa.
Hayo si maneno yangu, ila hii story nimetumiwa kwenye e-mail...mimi huwa siammini sana story za kutumiwa kwenye e-mail bila kuwa na majina, zaidi ya kufowardiana tu...ila hii ina kitu, tupia comment yako hapa tuijadili, afu na mie ntasema nilicho-observe...Karibu!
1 comment:
Asante mama X kwakuturushia hii kali. Naona uchungu sana kwa unyama alotendewa huyo malaika kama ni story ya kweli.
Kwakweli sina mengi zaidi yakuomba wamiliki wa Nursery wangeanzisha angalau baby care kuanzia miezi 7 hivi ili kusaidia baadhi ya watu wenye uwezo wa kupeleka watoto wao hapo.
Kwakweli hali ni mbaya kwa huu uchafu aloufanya huyo dada, nawaza sijui mtoto huyo kasalimika na uambukizwa magonjwa ya huyo katili?
Mtoto ameteseka sana kama mwanamke anaeteseka kila mwezi? Masikini mtoto mungu amuepushie maradhi yote.
Hongera kwa wazazi kuwa na subira kumnusuru huyo dada maana watu tunatofautiana hapo ingekuwa habari nyingine. Yaani nimechefuka sana nimebaki namuangalia kiumbe wangu nafananisha sipati jibu.
Basi hayo ndo mawazo yangu.
Mama Felista wa Norway.
Post a Comment