Thursday, May 24

Unamwekea mwanao akiba?

Hebu tujuzane, Hivi umeshawahi kufikiria kumwekea mwanao akiba?
Je unajua umuhimu wa kumuwekea mwanao akiba?
Ni wazazi wangapi wamewawekea watoto wao akiba aidha benki, mchagoni au kwenye kibubu?
Inawezekana hufahamu akiba ni kitu gani hebu tujuzane kwanza maana ya akiba.
Akiba: Ni kiwango fulani cha pesa kinachowekwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Haijalishi akiba inawekwa wapi, popote pale ni akiba.
Dunia ya leo hatujui kesho yetu. Wazazi ni muhimu kuwawekea watoto wetu akiba. Ebu imagine umfungulie mwanao akaunti ya benki halafu kwa kila mwezi umwekee 20,000 tu. Je akifika umri wa shule utakosa ada ya kumlipia shule nzuri? Kama unaona ni ngumu kwenda kupanga foleni benki kila mwezi benki unaweza kuweka standing order ili hela itoke kwenye account yako iende kwenye akaunti yake moja kwa moja.
Inawezekana huna mshahara ila una vitega uchumi vingine. Je umejiandaaje kwa ajili ya baadaye ya mtoto wako?
Mfano una nyumba tatu umepangisha, moja kati ya hizo unaweza ukatumia kodi yake kwa ajili ya kusave kwenye akaunti za watoto wako.
Tujijengee utamaduni wa kuwawekea akiba watoto wetu. Kesho yetu hatujui itakuwaje, tutumie pesa vizuri huku tukiwafikiria watoto wetu kesho yao. Kama tunawapenda watoto wetu tuwe na utaratibu wa kuwawekea akiba. 
Wahenga walisema Akiba Haiozi.

Je umemwekea mwanao akiba wapi? Ebu washirikishe wazazi wenzako katika hili.


Nimeona comment ya mdau anavyomaliza akiba ya mtoto - Unawezaje kuhakikisha huvunji kibubu cha mtoto? - tuongee wiki ijayo...

1 comment:

Anonymous said...

Umesema kweli ma dear, mimi nina juhudi sana kumwekea mwanangu, ila bahati mbaya huwa kila baada ya muda naitumia yote. Itabidi nijifunze kuto kutoa kabisa hela katika akaunti ya mwanangu.